USTAWI.

 

 USTAWI.

NINI MAANA YA USTAWI?

·         Ni Maisha Ya Kuondokana Na Uhitaji, Yaani Ni Maisha Ya Utoshelevu,

·         Ustawi Maana Yake Ni Utimilifu Wa Mtu, Pasipo Ustawi Bado Haujatimia.

·         Ustawi Maana Yake Umeufikia Wito Ambao Mungu Amekuumbia, Mungu Alimuumba Mwanadamu Kwa Sura Na Mfano Wake, Kwa Kusudi Gani?. Mungu Ali Kuumba Ili Afanane Naye. Katika Mungu Hakuna Labda Labda Bali Kuna Utimilifu.

Biblia Inasema Nini Kuhusu Ayubu? Ayubu Alikuwa Mtu Mkamilifu, Nini Maana Ya Ukamilifu?.  Maana Yake Alikuwa Ni Mtu Aliyestawi. Alikuwa Na Watoto, Wanyama Na Watumwa Walio Mzunguka Wa Kiume Na Wakike. Ustawi Maana Yeke Ni Utimilifu Wa Mtu. Ayubu 1:1 “Palikuwa Na Mtu Katika Nchi Ya Usi, Jina Lake Alikuwa Akiitwa Ayubu; Mtu Huyo Alikuwa Mkamilifu Na Mwelekevu, Ni Mmoja Aliyemcha Mungu, Na Kuepukana Na Uovu.”

Unapo Sema Mtu Huyu Ni Mkamilifu Inamaana Ameweza Kufikia Chanzo Cha Kuumbwa Kwake.

Ustawi Maana Yake Ni Kufikia Mwisho Yaani Kufikia Utimilifu Wa Maisha.

Ustawi Maana Yake Ni Kufikia Kilele Cha Maisha Yako, Kama Haujafikia Hicho Kilele Inamana Kuwa Haujastawi Bado.

Isaya 1:19 “Kama Mkikubali Na Kutii Mtakula Mema Ya Nchi;” Hii Inamaana Kuwa Ukikubali Na Kutii Ndipo Utaweza Kufikia Katika Mraba Wako. Kila Mtu Ana Mraba Wake Wa Kupiga Mbio Ili Kufikia Ustawi Wake.

Ustawi Si Kwa Ajili Ya Mtu Fulani Tu, La! Bali Ni Kwa Kila Mmoja Aliyeumbwa Na Mungu. Kwa Nini Wengine Wanastawi Na Wengine Hawastawi?.  Inategemeana Na Mitazamo Yao.

Chanzo Cha Uovu Wote Huku Duniani Ni Watu Kupenda Pesa. Tatizo Sio Pesa Bali Ni Wanadamu Wanapenda Pesa.

Ustawi Maana Yake Ni Pesa Inakupenda Wewe Yaani Uumbaji Unakupenda. Haujaumbwa Ili Uupende Uumbaji Bali Ni Uumbaji Ukupende Wewe Kwa Sababu Uumbaji Upo Ili Kukutumikia Wewe. Jua, Mwezi, Nyota, Mvua, Hewa, Nchi, Miti, Wanyama, Samaki N.K, Viko Ili Kukutumikia Wewe.

Kama Unafuga Wanyama Na Wanakufa Inamaana Kuwa Wanakuchukia.

Ustawi Maana Yake Ni Wewe Kufikia Kiwango Ambacho Uumbaji Unakupenda Wewe.

Kumbu Kumbu 28:1-2 “Itakuwa Utakaposikia Sauti Ya Bwana, Mungu Wako, Kwa Bidii, Kutunza Kuyafanya Maagizo Yake Yote Nikuagizayo Leo, Ndipo Bwana, Mungu Wako, Atakapokutukuza Juu Ya Mataifa Yote Ya Duniani; Na Baraka Hizi Zote Zitakujilia Na Kukupata Usikiapo Sauti Ya Bwana, Mungu Wako.”  Itakuwa Inamaana Gani? Maana Yake Ni Pale Utakapofikia Kilele Cha Maisha Yako; Unapo Zungumzia Hatima Maana Yake Umefika Eneo La Ukamilifu Katika Maisha Yako. Ukifikia Kileleni Ndipo Sasa Unaanza Maisha Bora Na Ndiyo Yanaitwa Ukamilifu.

“Itakuwa Utakaposikia Sauti Ya Bwana,” Ukifanya Kile Ulicho Ambiwa Ndipo Sasa Jambo Litatokea Kwako.

Utakapo Tii Sauti Ya Bwana Mungu Wako Ndipo Unaweza Kufikia Kilele Cha Mlima Wako Maana Yake Sasa Umehitimu Ki-Maisha Na Ndipo Kunakuwa Na Thawabu Kwa Sababu Umefanya Kile Ulichoambiwa. Ustawi Ni Thawabu Ambayo Unaipata Katika Maisha Baada Ya Kutimiza Ule Wajibu Wako. Ukifika Kileleni Hiki Ndicho Kinatokea Kwako Lakini Kama Sivyo Utaishi Kwa Kung’ang’ana, Kupambana Na Utakuwa Na Uhitaji.

Tatizo Sio Vitu Bali Ni Wewe Haujafikia Eneo Ambalo Mungu Amekuitia Uwe.

Kumbu Kumbu 28:2 “Na Baraka Hizi Zote Zitakujilia Na Kukupata Usikiapo Sauti Ya Bwana, Mungu Wako.” Wewe Haujui Hizo Baraka Zilipo Lakini Mungu Anajua Ziko Wapi, Ukifikia Kileleni Mwa Mlimwa Wako Baraka Ndio Zitakutafuta Na Si Wewe Unazitafuta.

Ukifikia Kilele Cha Wito Wako Hauombi Pesa Wala Chakula Bali Unakuwa Umepewa Kila Kitu, Haupiganii Kuishi Bali Kuna Mtu Anakuwa ana kupigania. Kufikia Kileleni Ni Utukufu Na Ndio Maana Yesu Akasema; Yohana 4:23 “Lakini Saa Inakuja, Nayo Sasa Ipo, Ambayo Waabuduo Halisi Watamwabudu Baba Katika Roho Na Kweli. Kwa Maana Baba Awatafuta Watu Kama Hao Wamwabudu.” Hii Inamaana Kuwa Waabuduo Halisi Wapo Kileleni Na Kwa Sababu Hiyo Wanasababisha Pesa, Watu N.K, Wawakaribie Au Viwakaribie Wao Kwa Sababu Wanavutia.

Kwa Nini Unang’ang’ana Katika Maisha Yako Leo? Kwa Sababu Haujafikia Kilele Cha Wito Wako, Wito Wako Si Kufukuza Mapepo Au Kuponya Wagonjwa, La! Bali Wito Ambao Tumeitawa Ni Kumtumaini Na Kumpendeza Mungu; Ukifikia Kipindi Hicho Ndipo Utampendeza Mungu Na Mungu Anawatafuta Watu Kama Hao. Watu Ambao Wamefikia Kiwango Hicho Hawaombi Chochote Kwa Mungu Bali Mungu Anawaambia Wafanye Nini Ili Waweze Kupata Thawabu Yao.

Ayubu 1:1 “Palikuwa Na Mtu Katika Nchi Ya Usi, Jina Lake Alikuwa Akiitwa Ayubu; Mtu Huyo Alikuwa Mkamilifu Na Mwelekevu, Ni Mmoja Aliyemcha Mungu, Na Kuepukana Na Uovu.” Huu Ndio Ukamilifu, Ayubu Aliwezaje Kuwa Mtu Mkamilifu? Alikuwa Mwelekefu, Nini Maana Ya Uelekevu?

·         “Mwelekevu” Alipenda Kujifunza Kujua Lipi Baya Na Lipi Jema.

·         “Aliyemcha Mungu” Ayubu Alikuwa Akimcha Mungu Yaani Alijitoa Kwa Matumizi Ya Mungu.

·         “Kuepukana Na Uovu.”Ayubu Alikaa Mbali Na Uovu.

Kwa Sababu Ya Hayo Ndipo Mungu Alimpa Ayubu Kustawi.

Ustawi Ni Thawabu Hauupiganii, Kuna Watu Wanafanya Kazi Kwa Bidii Sana Wakitumia Nguvu Nyingi Na Kuchoka Lakini Hawapati Kitu Chochote, Lakini Watu Wengine Wanastawi Kila Iitwapo Leo Hata Wasipofanya Kazi Ngumu, Kwa Nini? Kwa Sababu Wamefika Kilele Cha Mlima Wao.

Uliumbwa Kutimiza Kile Ambacho Mungu Alitaka Utimize Na Sio Kile Ambacho Wewe Unataka Kukitimiza, Mungu Alituumba Sisi Ili Kumfanya Yeye Awe Jinsi Alivyo Ili Kwamba Uumbaji Wote Lazima Usalimu Kwake, Hii Ndiyo Sababu Ya Uumbaji.

Mungu Hakukuumba Ili Utimize Mapenzi Yako Mwenyewe, La! Bali Kupitia Wewe Mapenzi Ya Mungu Yatimizwe. Wakati Mwingine Tunafanya Mapenzi Yetu Na Kufikili Kuwa Tunatimiza Mapenzi Ya Mungu, Lakini Sio Kweli Kwa Sababu Kama Ni Kweli Unatimiza Mapenzi Ya Mungu Katika Maisha Yako Hauwezi Kuwa Masikini. Ayubu Alipoteza Kila Kitu Kwa Muda Wa Miaka Mitatu Na Baada Ya Hapo Mungu Akamrejeshea Kila Kitu, Kwa Nini Kwa Sababu Aliamua Kutimiza Mapenzi Ya Mungu Katika Maisha Yake.

Hatufungi Ili Vitu Viende Vizuri Bali Tunafunga Ili Sisi Tuendelee Vizuri.

Usifunge Ili Kuifanya Biashara Yako Iende Vizuri Bali Funga Kwa Sababu Unataka Kufanya Vizuri Kwa Mungu Wako Ili Biashara, Pesa, Wateja Wakufuate.

Tunafunga Ili Tuondoke Katika Kuchelewa Na Kurejea Katika Reli Yetu Ili Tuweze Kwenda Haraka Na Kufikia Kule Ambapo Tunapaswa Kuwa. Mtume Paulo Akasema  Wafilipi 3:14 “Nakaza Mwendo, Niifikilie Mede Ya Thawabu Ya Mwito Mkuu Wa Mungu Katika Kristo Yesu.” Mwito Gani? Mwito Wa Ukamilifu Ili Kwamba Lolote Utakalo Tenda Upate Kustawi Na Hapa Ndipo Ustawi Unapoanza.

Chochote Utendacho Kitastawi, Kwa Nini? Kwa Sababu Umeufikia Wito Wako, Hauwezi Kustawi Kama Haujaufikia Wito Wako, Bali Utastawi Baada Ya Kuufikia Mwito Wako.

Mwito Mkuu Ni Kwa Wale Ambao Wamestawi; Usifunge Ili Duka Lako Lichanue, Wala Usifunge Na Kuomba Kwa Sababu Unataka Kupanda Cheo Kazini, La Wewe Funga Na Kuomba Ili Uungamanike Na Wito Wako.

Daniel Na Wenzake Hawakuomba Ili Wapande Cheo, Hapana! Bali Walifunga Na Kuomba Ili Wajiungamanishe Na Wito Wao Na Kitu Gani Kilitokea? Walichukuliwa Katika Kiwango Cha Heshima Katika Ule Ufalme.

Kila Mtu Anawito Wake Jiungamanishe Na Wito Wako Na Ujitoe Kwa Bwana Wa Mabwana Ndipo Utakuwa Umeshinda.

Ustawi Ni Kwa Ajili Ya Kila Mmoja, Ustawi Unaendana Na Mtu Ambaye Tayari Anaufahamu Wa Kile Alicho Umbiwa.

Kila Mmoja Wetu Anaweza Kufanya Maisha Yawe Bora Ikiwa Ukifahamu Maana Ya Ustawi. Watu Wanaangalia Sana Vitu, Wewe Angalia Wito Wako Ili Uweze Kustawi.

Kama Unataka Kukaa Katika Mstari Wako Kuelekea Wito Wako Unaweza Kuendelea Kufunga Mpaka Usikie Sauti Ya Bwnaa.

Yohana 14:13 “Nanyi Mkiomba Lo Lote Kwa Jina Langu, Hilo Nitalifanya, Ili Baba Atukuzwe Ndani Ya Mwana.” Unapo Chanua Anayepewa Utukufu Ni Mungu Wa Mbinguni Na Si Wewe, Kwa Nini? Kwa Sababu Mbingu Itasema Ulicho Kiumba Kimetimiliza Kile Ambacho Umekiumbia. Utakapo Fikia Ustawi Mbingu Itamsifu Mungu Na Ibilisi Pia.

Mungu Anapenda Kuwastawisha Watu Kwa Maana Anapo Wastawisha Si Kwa Ajili Yao Bali Ni Kwa Ajili Yake Mwenyewe Lakini Yeye Anazo Kanuni Za Kuwastawisha Watu.

Watu Wengi Ni Masikini Kwa Sababu Wanafikili Kile Walichonacho Ndio Kinaweza Kuwafanya Wawe Matajiri, Lakini Ukweli Ni Kuwa Sio Kweli. Pesa Inaweza Ikakuelezea Wewe Ni Nani, Kama Ni Masikini Au Tajiri. Mara Zote Pesa Inapenda Kwenda Mahali Ambapo Tajiri Yupo, Utajiri Sio Pesa Bali Ni Tabia, Na Maisha Ya Ustawi Ni Thawabu.

Kama Mtu Anatabia Ya Utajiri Mahali Popote Pale Utakapo Mpeleka Bila Kumpa Chochote Lakini Baada Ya Muda Mfupi Atakuwa Tajiri, Utajiri Si Pesa Bali Ni Tabia, Je! Wewe Unatabia Gani?.

Kumbu Kumbu 28:3 “Utabarikiwa Mjini, Utabarikiwa Na Mashambani.” Baraka Sio Pesa Wala Mahali Bali Ni Tabia Ya Mtu; Kama Umebarikiwa Basi Umebarikiwa Hata Uende Wapi Utabarikiwa, Ukiwa Unatembea Na Wito Wako Hauhitaji Pesa Ili Ubarikiwe Bali Baraka Zinapaswa Kukufuata.

Acha Wito Wako Utokee Na Kukuendesha Ili Kukufikisha Kilele Cha Wito Wako na Utafurahia.

Wale Wote Ambao mmesoma ujumbe huu na kuuelewa nawaombea, Ukastawi Katika Ndoa Yako, Ibada Yako, Utajiri Wako, Ukastawi Na Katika Kila Eneo La Maisha Yako Likastawi Kwa Jina La Yesu.

 Mungu Akubariki.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

NGUVU YA DAMU YA YESU

VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU