MWANA MPOTEVU.
MWANA MPOTEVU.
Luka
15:11-32 “Akasema, Mtu Mmoja
Alikuwa Na Wana Wawili; Yule Mdogo Akamwambia Babaye, Baba, Nipe Sehemu Ya Mali
Inayoniangukia. Akawagawia Vitu Vyake. Hata Baada Ya Siku Si Nyingi, Yule Mdogo
Akakusanya Vyote, Akasafiri Kwenda Nchi Ya Mbali; Akatapanya Mali Zake Huko Kwa
Maisha Ya Uasherati……..”
Mwana
Mpotevu Alichukua Sehemu Ya Mali Inayomuangukia Na Kuondoka Nayo Lakini Pia
Alidhani Akiondoka Na Hiyo Mali Atakenda Kufanikiwa, Baba Yake Alipompa Hiyo
Mali Alikuwa Na Tumaini Kuwa Atazalisha Na Kupata Faida, Lakini Ikawa Ni
Kinyume Chake Kwa Maana Aliitapanya Hiyo Mali Na Akaishia Kula Na Nguruwe.
Maisha Ya Mwana Mpotevu, Hakujali Ubaadae Wa Kesho Yake, Bali Alichojali Ni
Kile Alichokipata Na Kukitumia. Mwana Mpotevu Aliijua Nafasi Aliyonayo Kwa Baba
Yake Na Ndio Maana Akaenda Na Kudai Haki Yake.
Sifa
Za Mwana Mpotevu:
1.
Alikuwa Ni Mtu Wa Kuzingatia, Alijua Kwa Baba Yake Kuna Kila Kitu Na Yeye Ni
Sehemu Ya Hiyo Mali, Akilini Mwake Alijua Kuwa Lazima Achukue Kile Kinacho
Muangukia.
2.
Mwana Mpotevu Hakukataliwa, Maana Hata Alipokwenda Kwa Baba Yake Alipewa Kama
Alivyoomba Na Hata Alipoorudi Alipokelewa.
3.
Mwana Mpotevu Hakubishana Na Baba Yake. Alipokwenda Kuomba Mali Alipewa Na Hata
Alipokuwa Akirudi Baba Yake Alimpokea Vyema.
Kwako
Wewe Mwana Wa Mungu Leo Hii Ambaye Upo Nyumbani Mwa Bwana Ni Lazima Uwe
Mzingatiaji Ili Upate Haki Yako, Lazima Uzingatie Huku Ukijua Katika Nyumba Ya
Bwana Wewe Ni Sehemu Katika Huo Ufalme Wa Mungu Kwamba Una Sehemu Na Haki Yako
Pia Katika Nyumba Ya Mungu.
Itambue
Nafasi Yako, Dai Haki Yako Ili Upate Kuishi Maisha Yaliyo Na Utele Huku
Duniani.
Changamoto
Ya Mwana Mpotevu?
1.
Aliamua Kuondoka Katika Nafasi Yake Kwa Hiari Yake Mwenyewe Na Kwenda Mbali,
Alijua Atafanikiwa Na Ikawa Tofauti.
2.
Mwana Mpotevu Aliishi Maisha Ya Ugenini, Maisha Yasiyo Halisi Wala Hakukusudiwa
Na Baba Yake.
Walokole
Wa Siku Wa Leo Kuna Maisha Tunaishi Ambayo Siyo Ya Uhalisia, Uhalisia Maana
Yake Ni Nini? Ni Kuishi Sawa Na Vile Ambavyo Mungu Amewakusudia. Kuna Makusudi
Na Mpango Wa Mungu Kwako, Mungu Alikusudia Wewe Uishi Lakini Baada Ya Kuishi
Katika Kusudi Badala Yake Tunaishi Ugenini Yaani Mbali Na Makusudi Ya Mungu
Kwako. Mpango Wa Mungu Kwako Ni Kwa Wewe Kuishi Sawa Sawa Na Makusudi Ya Mungu
Aliyo Kukusudia.
Kwenye
Nyumba Ya Baba Yetu Kila Mmoja Ana Nafasi Yake, Cha Mshingi Ni Wew Uijue Nafasi
Yako Na Ufanye Kazi Katika Hiyo Nafasi Yako Ili Uweze Kuziona Baraka Zako. Je,
Wewe Nafasi Yako Ni Ipi? Itambue, Itendee Kazi Na Usimame Katika Hiyo Nafasi
Yako.
Kwenye
Nyumba Ya Bwana Kila Mmoja Ana Kipawa Chake Ambacho Ni Cha Pekee Na Hakifanani
Na Wengine, Kwenye Nyumba Ya Bwana Huna Haja Ya Kumuonea Wivu Mtu Mwingine Na
Usidhani Kwamba Cha Kwake Ni Bora Kuliko Cha Kwako Huo Ni Uongo Wa Shetania
Mbao Anautumia Ili Kutaka Kukutoa Katika Nafasi Yako. Usikubali Ibilisi Akutoe
Katika Nafasi Yako Kwa Wewe Kuishi Maisha Ambayo Si Halisi, Upeke Wako Ni Wa
Thamani Sana Mbele Za Mungu.
Kaka
Mkubwa:
Luka
15:11-32 “Akasema, Mtu Mmoja
Alikuwa Na Wana Wawili; Yule Mdogo Akamwambia Babaye, Baba, Nipe Sehemu Ya Mali
Inayoniangukia. Akawagawia Vitu Vyake. Hata Baada Ya Siku Si Nyingi, Yule Mdogo
Akakusanya Vyote, Akasafiri Kwenda Nchi Ya Mbali; Akatapanya Mali Zake Huko Kwa
Maisha Ya Uasherati……..”
Kaka
Mkubwa Hakujitambua Na Hali Yake Ya Kutokujiambua Ikamfanya Akawa Na Wivu Na
Ndugu Yake. Mtu Asipojitambua Lazima Wivu Na Roho Mbaya Iinuke Kwake.
Kaka
Mkubwa Hakutambua Nafasi Yake Katika Familia Yao. Hakutambua Kuwa Katika Nyumba
Ya Baba Yake Kuna Haki Yake.
Mtu
Wa Mungu Fika Mahali Ujitambue Wewe Ni Nani Kwa Maana Usipojua Haki Yako Kwa
Baba Yako Wa Mbinguni, Kuna Vitu Vitainuka Kwako Ambavyo Si Vizuri Na
Ukashindwa Kuipata Hiyo Haki Yako, Pata Kujijua Wewe Ni Nani Ili Uweze
Kuvishinda Vitu Vibaya Vitakapo Inuka.
Mungu
Yupo Kwa Ajili Ya Kumbariki Na Kumpa Kila Mmoja Haki Yake, Jitambue Ili Uweze
Kuchukua Haki Yako.
Ukijitambua
Wewe Mwenyewe Ndipo Utaanza Kuishi Maisha Ya Uhalisia. Jifunze Kuishi Maisha Ya
Uhalisia; Maisha Ya Uhalisia Ni Yapi? Mathayo 6:33 “Bali Utafuteni Kwanza Ufalme Wake, Na Haki Yake; Na Hayo Yote
Mtazidishiwa.”
USIPOTENDA VYEMA DHAMBI IPO.
Mungu Alituumba Tukiwa Waaminifu Lakini Yako
Yaliyofanyika Kwetu Hata Yakatufanya Tukawa Sio Wakamilifu. Sikio Ndio
Linaendesha Maisha Yako, Ukisikia Vizuri Utaona Vizuri Na Utamiliki Kizuri
Lakini Ukisikia Vibaya Utamiliki Vilivyo Vibaya.
Mwanzo 4:7 “ Kama Ukitenda Vyema,
Hutapata Kibali? Usipotenda Vyema Dhambi Iko, Inakuotea Mlangoni, Nayo
Inakutamani Wewe, Walakini Yapasa Uishinde.”
Nini Maana Ya Kutotenda Vyema? Ni Kutokutii
Maagizo Ya Mungu Kama Yalivyotolewa.
Kitu Gani Kinamfanya Mtu Asitende Vyema? Ni
Maamuzi Ya Mtu Binafsi; Kutenda Mema Au Mabaya Kupo Katika Maamuzi Ya Mtu,
Lakini Mara Zote Angalia Sikio Lako Limesikia Nini, Biblia Inasema, “Usimpe Ibilisi Nafasi” Kwa
Maana Ukimpa Tu Atakusikizisha Yaliyo Mabaya Ili Na Wewe Utende Yaliyo Mabaya.
Yoshua 24 “Nanyi
Kama Mkiona Ni Vibaya Kumtumikia Bwana, Chagueni Hivi Leo Mtakayemtumikia;
Kwamba Ni Miungu Ile Ambayo Baba Zenu Waliitumikia Ng’ambo Ya
Mto, Au Kwamba Ni Miungu Ya Wale Waamori Ambao Mnakaa Katika Nchi Yao; Lakini
Mimi Na Nyumba Yangu Tutamtumikia Bwana.” Hii Inamaana Kuwa Hata Kumwabudu Mungu
Haulazimishwi, Biblia Ipo Ili Kukupa Wewe Kujua Njia Hii Inaenda Upotevuni Na
Hii Inaenda Uzima Wa Milele, Ukiamua Njia Mbaya Mungu Anakusubiri Siku Ya
Mwisho Na Ukitenda Vyema Utaishia Uzima Wa Milele.
Madhara Ya
Kutokutenda Vyema; Utafukuzwa Kutoka Katika Nafasi Yako Na Ardhi Itakuwa
Haikupi Mazao, Yaani Utakuwa Kama Kaini, Kila Kitu Unachokifanya Kinakuwa
Hakifanikiwi. Mwanzo 4:11-15 “Basi
Sasa, Umelaaniwa Wewe Katika Ardhi, Iliyofumbua Kinywa Chake Ipokee Damu Ya
Ndugu Yako Kwa Mkono Wako; Utakapoilima Ardhi Haitakupa Mazao Yake;
Utakuwa Mtoro Na Mtu Asiye Na Kikao Duniani.” Kaini Alilaaniwa
Kwa Kutokutenda Vyema Na Aliye Mlaani Ni Mungu Mwenyewe Na Si Mwanadamu.
Usipotenda Vyema Unakuwa Mtu Wa Kuonewa, Mwanzo 4:14 “Tazama, Umenifukuza Leo Katika Uso Wa
Ardhi, Nitasitirika Mbali Na Uso Wako, Nami Nitakuwa Mtoro Na Mtu Asiye Na
Kikao Duniani; Hata Itakuwa Kila Anionaye Ataniua.”
2.
Ufanye Nini Ili Utende Vyema?
·
Ishi Maisha Matakatifu Ya Kumpendeza Mungu,
·
Lisha Roho Yako Kila Iitwapo Leo, Neno La
Mungu Likae Ndani Yako Kwa Wingi Kwa Maana Neno Linabadilisha.
·
Uwe Mtii, Kubali Kujitoa Na Uwe Mwaminifu.
·
Ishi Kama Mtoto Mchanga.
KUZINGATIA
Kuzingatia Ni Nini? Ni Ile Hali Ya Kutenda Sawasawa Na Kile Ulicho Kisikia Au Ulicho
Kiona. Kama Hautendi Sawa Sawa Na Kile Ulichokiona, Kusikia Au Kuelekezwa
Unakuwa Ni Mtu Asiye Zingatia.
Kuzingatia Au Kutokuzingatia, Unapofanya Moja
Kati Ya Hayo Kuna Matokeo Lazima Uyapate.
Nini Kitatokea Utakapozingatia?
Kumbukumbu La
Torati 28:1 “Itakuwa Utakaposikia Sauti Ya Bwana, Mungu
Wako, Kwa Bidii, Kutunza Kuyafanya Maagizo Yake Yote Nikuagizayo Leo, Ndipo
Bwana, Mungu Wako, Atakapokutukuza Juu Ya Mataifa Yote Ya Duniani;”
Biblia Inasema Utakaposikia Sauti Ya Bwana Kwa Bidii, Neno “Bidii” Maana
Yake Inaonyesha Msimamo Wa Kuzingatia. Bwana Atakapo Kutukuza Maana Yake
Anakupa Kibali Mbele Za Watu Na Mbele Zake Yeye Mwenyewe. Hivyo Siku Zote Mtu
Anayezingatia Atapata Matokeo Chanya.
Kusudi La Kuumbwa Kwako Ni Nini?
Mwanzo 1:28 “Mungu Akawabarikia, Mungu Akawaambia, Zaeni, Mkaongezeke, Mkaijaze
Nchi, Na Kuitiisha; Mkatawale Samaki Wa Baharini, Na Ndege Wa Angani, Na Kila
Kiumbe Chenye Uhai Kiendacho Juu Ya Nchi.” Mungu
Aliweka Muongozo Huu Ili Mimi Na Wewe Tuufuate Ili Tupate Kuwa Sawa Na Ndivyo
Mungu Alivyotaka Tuwe.
Kuna Mambo Matatu Tunajifunza Kupitia Mstari
Huu:-
1. Kuzaa Na Kuongezeka,
2. Kumiliki Na Kutawala,
3. Kutunza.
Ukiangalia Haya Mambo Matatu Ndiyo Yamebeba
Biblia Tuliyonayo Leo Hii, Huu Ndio Muongozo Ambao Mungu Aliuweka Ili Sisi
Wanadamu Tuweze Kutembea Katika Huo.
Ulimwengu Unapitia Katika Hali Ngumu Sana Leo
Hii Kwa Sababu Ya Nini? Ya Kumiliki Na Kutawala. Inapofika Katika Hatua Hii Mtu
Anaweza Kutoa Hata Roho Ya Mwenzie Ili Apate Nafasi Ya Kumiliki Na Kutawala.
Lengo La Mungu Kukuweka Ulimwenguni Ni Ili
Wewe Upate Nafasi Ya Kumiliki Na Kutawala Hayo Aliyoyaumba, Ndio Maana Akaweka
Wanyama, Miti, Bahari Na Kila Kitu Unachokiona Na Kisha Akakuweka Wewe Ili
Upate Kumiliki Na Kutawala.
Je! Wewe Umeweza Kuchukua Nafasi Yako Ambayo
Mungu Alikuwekea Kabla Ya Kuumbwa Kwa Ulimwengu?. Je? Unatawala Na Kumiliki?
Watu Wengi Hawako Kama Vile Ambavyo Mungu
Amewakusudia Na Ndio Maana Wanapita Katika Changamoto Mbali Mbali, Kuna
Umasikini Na Uhitaji Haya Yote Ni Kwa Sababu Hatukuzingatia Kile Ambacho Mungu
Ametukusudia.
Kutunza Kile Ambacho Mungu Amekupa, Hapa
Ndipo Kuna Shida.
Inawezekana Wewe Ni Kiongozi Serikalini,
Sekta Binafsi, Kanisani N.K Hiyo Nafasi Uliyonayo Ni Ya Muhimu Sana, Usipo
Itunza Kuna Mtu Anaisubiria Kwa Hamu Sana, Utawezaje Kuitunza? Ni Kwa Kufuata
Maagizo Na Masharti Ya Hiyo Kazi, Ukienda Kinyume Na Hayo Utaikosa Hiyo Nafasi
Na Ataichukua Mtu Mwingine, Ni Nani Huyo?. Mwanzo 3:4 “Nyoka Akamwambia Mwanamke, Hakika Hamtakufa,” Mungu
Aliwaambia Wasile Tunda Lakini Nyoka Akamwambia Wale Hawatakufa, Kazi Ya
Ibilisi Ni Kukutoa Katika Nafasi Yako Ili Akae Yeye.
Ukiona Kuna Mtu Anataka Kukutoa Katika Nafasi
Yako Huyo Mtu Ndiyo Adui Yako Kwa Maana Amesimama Badala Ya Ibilisi.
Matokeo Ya Kutokuzingatia; –
1. Utaona Mpambano,
2. Magonjwa Na Maradhi Yatakuwa Ni Sehemu Ya
Maisha Yako,
3. Utaona Kutenga Au Kufukuzwa Mbali Na
Kusudi La Mungu Kukuumbia Huku Duniani.
Maoni