KUONGOZWA NA ROHO

 KUONGOZWA NA ROHO.


Maombi ni lazima, tumehimizwa na muumbaji kuomba, Kwa kila mwamini anapaswa kuwa na mambo yafuatayo:-

1.      Afanye kazi,

2.      Awe na umiliki juu ya nchi,

3.      Azalishe,

4.      Aombe,

5.      Ashuhudie,

6.      Aabudu,

7.      Lazima awe mtoaji,

8.      Lazima uwe na upendo, penda uumbaji,

9.      Lazima asamehe na atubu,

10.  Ahakikishe anatunza wito wake.

 

Ukiyaweka haya pamoja ndipo unakuwa yule ambaye Mungu anampenda,

 

1 Wakorintho 2:10 “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.”

Mungu ametupa ufunuo kupitia roho wake, ufunuo ni nini? Maana yake ni kugundua mambo yaliyo sirini, maswala ya kiroho ukiyagundua yale yanayo kuhusu wewe, Mungu au ya ibilisi yaliyo katika roho hiki ndicho tunakiita ufunuo inamaana yamefunuliwa kwako.

Biblia inasema “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.” Hii inamaana kuwa Mungu amekujulisha au amekusaidia kujua mambo yake kupitia roho. Unapo gundua mambo ya Mungu yale yaliyofichwa na usiyoyajua yanaweza kuwa mazuri au mabaya makubwa au madogo lakini Mungu amekujulisha kupitia roho huo ndio unaitwa ufunuo.

 

1 Wakorintho 2:11 “Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.”

 

Hakuna aujuaye moyo wako kwa sababu ni wa kwako, chochote kilicho cha kwako ambacho hakijawahi kufunuliwa kwa wengine inamaana ni cha kwako na anayekijua ni wewe mwenyewe.

Hakuna anayekujua wewe kuliko unavyojijua mwenyewe sasa acha kuwawazia watu kwa maana wewe ndiye unaye jijua mwenyewe, unakuta mtu anabeba vitu vingi kuhusu watu lakini Biblia inasema hakuna ayafahamuye mambo ya wanadamu pasipo yeye mwenyewe, jitazame wewe.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

NGUVU YA DAMU YA YESU

VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU