Lampard arudi Chelsea kwa muda

Frank Lampard ameteuliwa kuwa kocha wa muda wa Chelsea FC ambapo atainoa timu hiyo hadi mwisho mwa msimu.


Lampard anarudi tena Darajani kama kocha baada ya kuitumikia kwa mafanikio akiwa mchezaji akishinda mara tatu Ligi Kuu ya England pamoja na taji moja la UEFA.

Lampard ataongoza Chelsea katika mchezo wa robo fainali wa Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Aprili 2 mwaka huu Chelsea ilivunja mkataba na Graham Potter kutokana na matokeo yasiyorodhisha, na sasa itakuwa katika kibarua cha kutafuta kocha wa kudumu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

NGUVU YA DAMU YA YESU

VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU