AINA ZA MAOMBI
*AINA ZA MAOMBI.*
*1. MAOMBI YA KUWAOMBEA WATU WENGINE (MAOMBEZI).*
-Kwa mtu aliyeokoka ni lazima uwaombee watu wengine, mojawapo na sababu inayomfanya Mungu ajibu maombi yako lazima usiwe mbinafsi jali na wengine kwa kuwaombea.
-1 SAMWEL 12:23 Walakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka
-EZEKIEL 22:30 Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.
31 Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.
FAIDA YA MAOMBI YA KUWAOMBEA WATU WENGINE (MAOMBEZI).
-Yanaimarisha kanisa katika misingi ya Umoja na Upendo.
-Inajenga nafasi nzuri ya Mungu kuanza kutenda kwako.
-Yanawajenga watu wengine waweze kusimama vizuri kwenye wokovu (mfano maombi ya washirika juu ya viongozi wa kanisa).
-Yanamfanya Mungu ajibu na kusikia maombi (hasa pale mtu anapokuwa ametenda dhambi au hajaokolewa, lakini ukaomba toba juu yake Mungu atamsamehe na kumsikia.
-Yanaponya na kufungua watu waliofungwa na nguvu za giza.
HASARA ZA KUTOKUWAOMBEA WATU WENGINE.
-Maombi yako kuchelewa au kutokujibiwa kwasababu ya ubinafsi.
-Kunapunguza nguvu ya uponyaji na miujiza kwasababu hakuna wa kuombea wengine wenye matatizo.
-Kunapunguza upendo na nguvu za Roho Mtakatifu ndani ya kanisa.
-Ni dhambi kwa kutokuwaombea wengine hauwezi kuurithi ufalme wa Mungu. (1 Samwel 12:23).
*2.MAOMBI YA TOBA NA REHEMA.*
-Maombi haya hufanywa kutokana na maovu fulani yaliyotea, au dhambi au makosa, kwa mtu binafsi, familiya, kanisa au taifa na baada ya kufanyika adhabu iliyopangwa katika juu ya maisha ya hao watu au uyo mtu, Mungu hugairi.
-2 NYAKATI 7 :14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
-Isaya 1:18 Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
-Isaya 43:25 Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.
-Mithali 28:13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
FAIDA ZA MAOMBI YA TOBA NA REHEMA.
-Kuna mfanya Mungu aachilie rehema na msamaha juu ya waombaji.
-Kuna fungua nafasi ya Mungu kujibu maombi yako(maana Mungu hajibu maombi ya wenye dhambi).
-Kuna mfanya Mungu aachilie uponyaji na uzima(hasa kwa matatizo yaliyotokana na dhambi mfano magonjwa).
-Kuna rejesha vyote vilivyotekwa kutokana na dhambi kama ni mafanikio, baraka na nk.
-Yanauisha na kuamsha kwa upya Nguvu za ROHO mtakatifu ndani ya mtu binafsi, kanisa au taifa.
HASARA ZA KUTOKUOMBA MAOMBI YA TOBA NA REHEMA.
-MUNGU hawezi kusikia maombi yako(hasikiagi maombi ya wenye dhambi:Isaya 59)
-Kuna kufungua mlango wa matatizo mbalimbali mfano magonjwa, kutokufanikiwa, umaskini, kuchukiwa na nk.
-Kunaondoa uwepo wa Roho Mtakatifu na nguvu zake iwe kwa kanisa au mtu binafsi.
-Hautaurithi ufalme wa Mungu (kwa sababu huna utakatifu).
-Utaishi maisha ya kukosa amani na furaha (ndani yako huna nguvu ya kustahimili majaribu na vikwazo mbalimbali).
*3.MAOMBI YA SHUKRANI.*
-Kwa mambo mengi makuu ambayo Mungu amekutendea, hata uhai wako, afya, elimu, ndoa, watoto, uchumi majaribu na mapito mbalimbali ambayo Mungu amekusaidia.
-Yohana 11: 41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.
-1 WATHESALONIKE 5 :18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
-Zaburi 92:1 Ni neno jema kumshukuru BWANA, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu.
-Zaburi 50:23 Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.
FAIDA YA MAOMBI YA SHUKRANI :
-Yanatoa nguvu na uwezo wa kustahimili majaribu na changamoto
mbalimbali.
-Yanampa Mungu sifa utukufu zaidi.
-Yanamuaibisha shetani na kudhihirisha ukuu wa Mungu.
-Yanakuza viwango vya imani, hasa pale unavyomshukuru Mungu kwa mambo yanayokuja(Kwa maana nyingine yanamfanya Mungu ajibu maombi yako kwa sababu umeonyesha imani kuwa anaweza.
-Yanamfanya Mungu ajibu maombi yako zaidi ili uzidi kumshukuru,(Mungu anapenda kushukuriwa na kupewa utukufu :Zaburi 50:23 Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.)
HASARA ZA KUTOKUMSHUKURU MUNGU.
-Kuna chelewesha au kukamisha majibu ya maombi yetu.
-Kuna punguza ulinzi wa Mungu juu ya maisha yetu au juu ya vile tulivyonavyo.
-Kuna punguza viwango vya imani vya kumwamini Mungu hasa wakati tupo kwenye majaribu na changamoto mbalimbali.
*4.MAOMBI YA MAPATANO AU YA PAMOJA:*
(Maombi haya hupangwa kanisa au kikundi fulani kinachoamua kuomba kwa pamoja wanakubaliana kuomba na kufunga kwa pamoja).
-Matendo 1:14 Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.
-Matendo 2:42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.Maisha ya Waumini
Maombi haya ni kuungana pamoja na kuomba kwa pamoja
Mnajitoa kwa Pamoja kwa ajili ya kuombea jambo Fulani.
FAIDA YA MAOMBI YA MAPATANO.
-Yanatia nguvu ya kuomba, (hasa kama hupendi kuomba au wewe ni mvivu wa maombi).
-Yanajenga ushirika na ukaribu baina ya waombaji.
-Yanainua na kutiana nguvu hasa pale mmojawapo anapokuwa kwenye tatizo fulani.
HASARA ZA KUTOKUSHIKIRI MAOMBI YA MAPATANO.
-Kuna fungua mlango wa adui kwako kukuingiza kwenye majaribu (hasa roho za malipizi, wengine wanaomba ila wewe hauombi mfano kwenye kanisa, au kikundi fulani).
-Kuna muhuzunisha Roho Mtakatifu, wakati mwingine hupelekea kuchelewa kupata matokeo ya maombi yako.
-Kuna kupunguza kiu na shauku ya kuomba ndani yako.
*5.MAOMBI YA KUFUNGA.*
-Haya ni mojawapo ya maombi yenye nguvu kubwa na huleta matokeo makubwa sana kwa waombaji na hushusha nguvu za Mungu kwa kiwango kikubwa,kadri kadri unavyozidi kufunga muda mrefu ndio matokeo yanazidi kuongezeka na kuonekana.
-Mathayo 17:21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]
-Luka 4:1 Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,2 akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.
-Ester 4:16 Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.
-Zaburi 35:13 Bali mimi, walipougua wao, Nguo yangu ilikuwa gunia. Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga; Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu.
-Yona 3:7 Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng’ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji;8 bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake.10 Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.
Ziko aina mbali mbali za kufunga ila nitazungumzia aina kumi tu.
1.Aina yetu ya kwanza ni kufunga kwa kuvusha mlo mmoja ,kwa mtu aliyezoea kula Milo mitatu kwa siku anatakiwa kuacha kula mlo mmoja
2.Funga ya pili,kuvusha milo miwili saa 24 ,unaacha kula asubuhi na mchana unakula jioni hii ndio funga ambayo watu wengi huependelea kufunga
3.Kuvusha Milo mitatu yaani moja, kavu saa 24
4.Kuvusha Milo sita yaani mbili kavu saa 48
5.Kuvusha Milo 9,tatu kavu masaa 72
Hii ndio funga aliyoifanya Esta,
Esta 4:16 Uende ukawakusanye wayahudi wote waliopo hapa Shushani,mkafunge kwaajili yangu,msile wala kunywa,muda wa siku tatu,usiku na mchana,nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile,kisha nitaingia kwa mfalme,kinyume cha sheria,nami nikiangamia na niangamie.
6.Funga ya Danieli, kutokula vyakula vitamu, Danieli alifunga kwa kula mtama na maji Alifunga muda Wa majuma matatu, siku 21
Danieli 10:2,3
Katika siku zile, Mimi Danieli nilikua nikiomboleza muda Wa majuma matatu kamili
Sikula chakula kitamu,wala nyama,wala divai haikuigia kinywani mwangu
Wala sikujipaka mafuta kabisa hata majuma matatu kamili yalipotimia
7.Funga ya Yohana Mbatizaji,Alifunga kwa kula chakula cha aina moja tu nzige na asali
8.Funga ya lazimishwa hii ilimtakea Yona
Yona 1:17 Kisha Mungu akaamuru samaki mkubwa ammeze Yona,naye akawa tumboni mwa Samaki huyo kwa muda Wa siku tatu,usiku na mchana
Pia Matendo 27:33
“Karibu na alfajiri,Paulo aliwahimiza,wote wale chakula” *Kwa siku kumi na nne sasa mmekuwa katika Mashaka na bila kula,hamjala kitu chochote
Kuna watu ni waoga kufunga,wakati mwingine Mungu hutumia njia mbadala kama ya Yona na kina Paulo ili kuwafundisha kufunga
9.Funga ya Musa siku 40
10.Funga ya wazi kanisa au Taifa
FAIDA YA MAOMBI YA KUFUNGA:
-Yanaachilia nguvu za Mungu kwa uzito zaidi(kuna vitu vingine bila maombi ya kufunga havitokei).
-Yanainua viwango vya kiroho na nguvu za ROHO mtakatifu ndani ya mtu.
-Yanaleta majibu ya KiMungu kwa urahisi zaidi (kadri unavyozidi kufunga na kuomba ndivyo matokeo yanazidi kutokea).
-Yanatoa uwakika zaidi ya maamuzi yako:kuna maamuzi kwenye maisha yako juu ya kufanya jambo fulani, lakini usipoomba na kufanya huwezi kupata uwakika hasa wa lini, na nani na namna ya kulifanya.
HASARA ZA KUTOKUFUNGA.
-Kuna ondoa kiu na shauku ya kumtafuta Mungu zaidi.
-Kunapelekea kukosa nguvu na imani ya kusonga mbele hasa katika Nyakati ngumu.
-kunapelekea kuwa na matokeo hafifu kwakile ukiombacho kama wewe sio mtu wa kufunga na kuomba.
-Jambo la kujifunza ni hili. MUNGU hajibu maombi yako kwa vile umejitesa na kuacha kula. MUNGU anakujibu kwa vile umeitesa nafsi yako, ukainyima vingine na kumpa MUNGU nafasi kwanza. Wengine wanasema wamefunga ila bado hawana utulivu wa kusema na MUNGU. Wengine wanajinyima kula na kunywa ila hawaombi wakidhani kutokula na kunywa bila kuomba inatosha. HAPANA. Tesa nafsi yako kwa kubadilisha ule mfumo wa kawaida wa maisha na pata muda wa kutosha kusema na MUNGU. Kumbuka Yesu alienda nyikani bila kula wala kunywa ila zaidi kuitesa nafsi kwa kuinyima vile ilivyozoea katika maisha ya kawaida.
-Wengine wanafunga huku wanawaza mabaya na kutegemea kupokea majibu chanya kitu ambacho hakiwezekani. Wengine wanafunga na bado wanaendelea na utaratibu wa maisha ya kawaida,kwa mfano kutazama filamu, kusoma magazeti, kushika simu na kuchat na hawana muda wa kuutafakari ukuu wa MUNGU na kuutafuta uso wake. UTACHELEWA SANA KUONA MATOKEO. Acha maisha ya anasa na umtafute MUNGU kama kweli unataka kuona jambo jipya likitendeka.
*6.MAOMBI YA VITA.*
(Haya ni maombi kuharibu, kuvunja, kusambaratisha, kubomoa, kuteketeza, kuyeyusha, kung’oa na kuuwa kila nguvu za giza zinazotumwa kwetu au zinazokuwepo katika mazingira tunayotaka kuyatawala ili kufanya kazi ya Mungu)
-Waefeso 6:11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
-2 WAKORINTHO 10:3 Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
-Yeremia 51:20 Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;
-Yeremia 1:10 angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.
FAIDA YA MAOMBI YA VITA:
-Yanaleta urejesho wa vyote vilivyoibiwa na adui.
-Yanaangusha ngome na ufalme wa giza.
-Yanatupa nguvu mpya kashinda majaribu na kusonga mbele.
-Yanatup
a nguvu ya kushinda dhambi na vishawishi.
-Yanatupa nguvu ya kutimiza mapenzi na kusudi la Mungu.
MADHARA YA KUTOKUOMBA MAOMBI YA VITA.
-Unakosa nguvu ya kiroho ya kumshinda adui.
-Kuna mpa adui nafasi wa kutesa maisha yako na kuyaonea.
-Hautaweza kutembea katika nguvu za Mungu na mapenzi yake.
*7.MAOMBI YA KUKESHA(MKESHA).*
(Unaweza kukesha na kuomba kuanzia usiku mpaka asubuhi au ukaingia kwenye maombi usiku wa manane au ukaomba alfajiri).
-Luka 6:12 Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.
-Mathayo 26:41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho I radhi, lakini mwili ni dhaifu.
-Marko 1:35 Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.
FAIDA ZA MAOMBI YA KUKESHA.
-Yanakuza nguvu ya kuomba ndani ya maisha ya mwamini.
-Yanatusaidia kushinda majaribu na changamoto mbalimbali.
-Yanajenga maisha yetu na kesho yetu kuwa bora zaidi.
-Yanauisha na kutupa nguvu na kiu ya kumtumikia Mungu zaidi.
HASARA ZA KUTOKUOMBA MAOMBI YA MKESHA.
-Mara nyingi lazima utakuwa mvivu wa kuomba.
-Kunapelekea kuingia kwenye majaribu au kushindwa kushinda majaribu na vikwazo.
-Kuna pelekea kutokutembea katika viwango kamili vya mapenzi ya Mungu.
*8.MAOMBI YA KUMLILIA MUNGU (KWA MACHOZI).*
(Unaweza kuomba maombi yako ukamlilia Mungu kutokana na ugumu au uzito wa tatizo husika au haja ya moyo wako).
-1 SAMWEL 1:10 Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba BWANA akalia sana.
-Ayubu 7:11 Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu; Nitanena kwa mateso ya roho yangu; Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu.
-2 NYAKATI 32:20 Na kwa ajili ya hayo Hezekia mfalme, na Isaya nabii, mwana wa Amozi, wakaomba, wakalia hata mbinguni.
FAIDA YA MAOMBI YA KUMLILIA MUNGU (MACHOZI).
-Yanashusha nguvu za Mungu kwa viwango vikubwa hasa wakati wa maombi.
-Yanajenga kiu na shauku ya kumtafuta Mungu.
-Yanajenga mazingira mazuri ya kujibiwa maombi yako hasa maombi ya toba na rehema.
HASARA ZA KUTOKUMLILIA MUNGU.
-Kuna vitu havitafanyika kwenye maisha yako mpaka umlilie Mungu kwa muda mrefu na kuomba.
KUMBUKA:UNAWEZA KUOMBA MAOMBI ZAIDI YA AINA MOJA KATI YA HAYA:
Maoni