UTOAJI
*UTOAJI MBELE ZA MUNGU UNAVYOWEZA KUKUFUNGULIA MLANGO MKUBWA WA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKO*
*Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya*
(1 Wafalme 17:16)
Siku ya leo tutafakari kwa kina ujumbe huu
*Kila kitu ni utoaji* na hakikisha unasoma na kuchukua hatua.
👉Yaani Kama hautoi basi pia hupokei. Na kama haupokei basi hutoi.
✅Utoaji ni daraja kati ya mafanikio yako na wewe ulipo. Utoaji ni mbegu, ambayo baadaye itakuzalia matunda.
◾Jiulize wewe unatoa nini?
◾ Unatoa kwa nani?
◾Unatoa wapi?
📌Watu waliofanikiwa tabia moja wapo inayofanya wafanikiwe ni utoaji.
✅ Kwa wale wasomaji wazuri wa biblia, imebainisha bayana kabisa kuwa, heri kutoa kuliko kupokea.
✅Kwa maana anayetoa atapokea na kuongezewa zaidi.
""Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya *Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea*
(Matendo ya Mitume 20:35)
📌Familia nyingi zinazoteseka kwenye ufukara ni familia ambazo huwa siyo watoaji.
✅Kama ulishawahi kuishi maisha ya kijijini utakubaliana na mimi.
✅Familia zenye hali nzuri kimaisha ni familia ambazo zinapokea na kukarimu wageni.
✅Kwa sababu kuna mahali wanatoa, basi huwa wanaopokea pia. Yaani wanaogezewa pale walipo toa.
*Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua*
(Waebrania 13:2)
✅Utoaji siyo lazima utoe pesa. Utoajia siyo lazima utoe kanisani.
📌Bali unaweza ukatoa chochote, sehemu yoyote, wakati wowote, Mahali ambapo Utaongozwa na Roho Mtakatifu
✅Kanuni hii ya utoaji, huwa haijalishi wewe ni nani, umetoka wapi? Umezaliwa wapi? Ni mzungu au mwafrika, bali kama wewe ni mtoaji basi lazima utafanikiwa tu.
✅Kuna watu wengi wanavipaji, lakini kwa sababu ya kutokujua kutoa ili vitumike kwenye madhabahu ya Mungu Vipaji vyao haviwezi kupokelewa kwenye jamii,kanisani nk
📌Chukulia mfano wa stoo iliyojaa vitu. Ili uweze kuweka au kuingiza vitu vingine vipya na vizuri ni lazima uvitoe vitu vya zamani vilivyo jaa kwenye stoo, ndipo upate nafasi ya kuweka vitu vipya.
📌Hivyo ndivyo watu wengi huwa hawaelewi maana ya utoaji.
✅Utoaji unakuwezesha wewe kuweza kupokea vitu vipya na vizuri zaidi. Unapotoa unaruhusu vitu vipya na vizuri viweze kupata nafasi.
✅Usipotoa maana yake stoo yako itakuwa imejaa vitu vya zamani na hakuna pa kuweka vitu vipya.
📌Kila mtu anacho cha kutoa. Toa chochote ulichonacho. Siyo lazima utoe pesa. Siyo lazima utoe vitu vya thamani sana. Unaweza ukatoa Muda wako au Nguvu zako.
📌Angali ulicho na uwezo nacho, toa.
*Mungu aliwaambia Wana wa Israel watoe ingawa walikuwa Jangwani*
📌Usifikiri kwamba labda ni watu fulani tu ndiyo wanaotakiwa kutoa, la hasha angalia kile ambacho unaweza ukatoa.
✅Hebu leo fanya zoezi hili nyumbani kwako, angalia kwenye kabati lako la nguo, begi lako au unapotunza nguo zako. Kama unanguo ambayo hujaivaa kwa mwaka mzima, hiyo nguo unahitaji umpe mwenye uhitaji.
📌 Unatakiwa uitoe, kwa kufanya hivyo itakusaidia wewe kupata nguo nyingine mpya na nzuri zaidi.
*Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya*
(Luka 5:38)
Mungu awabariki Sana Sana
Maoni