Akizungunza katika mkutano wa Siku ya Vijana Duniani jijini Lisbon Papa alisema kuwa mgando wa fikra wa baadhi ya watu “hauna manufaa”.
"Kwa kufanya hivyo unapoteza utamaduni halisi na utategemea itikadi ili kuungwa mkono. Kwa maana nyingine, itikadi inachukua nafasi ya imani,” aliongeza kusema. Papa pia amewashutumu vikali wale wote wanaokanusha mabadiliko ya tabianchi na anatazamiwa kuwa katika mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa wa COP28 baadae mwezi huu huko Dubai. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Papa kuhudhuria toka mikutano hiyo ianzishwe mwaka 1995.
Maoni