NGUVU YA DAMU : Damu ya Yesu ndiyo inayomfanya mwamini awe mtakatifu wa Mungu, hauwi mtakatifu pasipo Damu ya Yesu kukusafisha. Unahitaji damu ya Yesu kukusafisha ili uwe mtakatifu wa Mungu. Haki huja kupitia Neno lakini utakatifu huja kwa kupitia damu. Katika damu ndipo ukombozi ulipo, huwezi kutoka kwenye dhambi na uovu ambao unaokufanya usiwe mtakatifu pasipo Damu ya Yesu, ni kwa Damu pekee ndiyo itakufanya uwe mtakatifu wa Mungu na huo utakatifu ndio unamfanya Mungu avutiwe na wewe. Utakatifu wako ndio utakao mvutia Mungu lakini ili uupate ni lazima uipate Damu ya Yesu na hapo ndipo ukombozi ulipo. Nguvu inayo fukuza dhambi zote maradhi na magonjwa ni damu ya Yesu, kupitia Damu tunao ukombozi wetu, wokovu, utakatifu, tunakuwa washiriki wa mambo ya mbinguni. Ufunuo 12:11 “ Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa .” tunamshinda adui, maradhi na magonjwa kwa Damu ya Yesu, imo nguvu ndani ya hiyo Damu...
Maoni