Machapisho

JINSI YA KUMFANYA MUNGU AFURAHI.

Picha
  JINSI YA KUMFANYA MUNGU AFURAHI.   Biblia inasema Roho wa Bwana anatusaidia kumfanya Mungu afurahi. Pia anatusaidia kuomba sawa sawa na mapenzi ya Mungu, wakati mwingine tunafikiri kuwa tunajua kuomba na kumfanya Mungu asikie lakini tunapiga kelele tu. Tunaweza kufunga na kuomba kwa kitambo lakini Mungu hawezi kusikia kwa sababu wakati mwingine anasikia kelele. Tufanyaje ili kumsababisha Mungu asikie? Tunamfanya Mungu asikie pale tunapo omba sawa sawa na mapenzi yake.   1 Yohana 5:13-14  “Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu. Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.” Ukiomba sawa sawa na mapenzi ya Mungu YEYE anatusikia; kuna mapenzi kwa ajili ya mwaka huu, kwa ajili ya mwaka jana na kuna mapenzi kwa mwaka ujao na yako pia mapenzi ya Mungu kwa ajili yako. Yako mapenzi kwa ajili ya Tanzania sasa yapasa kuelewa, kwamba unataka kuo...

HABARI YA MSALABA.

Picha
   HABARI YA MSALABA. Tuko Kanisani kwa sababu ya imani yetu tuliyonayo na hatupo ili kusheherekea, tunakusanyika hapa kwa ajili ya imani ya Yesu Kristo ambayo ilianza na Ibrahimu, ni imani gani hiyo? Ya kumwamini muumbaji.   Kama Biblia inasema  “pasipo imani hauwezi kumpendeza Mungu”   njia pekee ya kumpendeza Mungu ni kukaa katika imani; kwa nini watu wanahangaika, wanateseka na wanang’ang’ana ili wapate chakula, wapate kodi au ada ya shule? Kwa sbabau wamekosa Imani ndani yao. Wafilipi 4:13 “ Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. ” Yupo Mungu anayekuwezesha kupata kile unacho kihitaji, lakini kama haumtumaini kamwe hautaweza kuishi vizuri hapa duniani.   Imani inamfanya mtu jinsi alivyo, je! Wewe unaamini nini? Tutayaona maisha yako. Imani tuliyomo ndani yake inaanzia pale msalabani na siyo mahali pengine. Ukitaka matatizo, mateso na maumivu yote yafikie kikomo ni pale utakapolijua Neno msalaba. 1 Wakorintho 1:18-19 “ Kwa sabab...