Machapisho

UMILIKI WA MWANADAMU

Picha
  Umiliki wa mwanadamu;  Hatuwezi kuzungumzia Baraka pasipo kuelewa nafasi ya mwanadamu; Nafasi ya mtu itamuhakikishia mtu huyo nini anachoweza kumiliki.   Mwanzo 1:26-27 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.”   Nafasi ya mtu ni lazima iungamane na muumbaji, pasipo hilo kumiliki ni kitu kigu mu kwa huyo mtu. B. Baraka ni nini? Ni neno lililotamkwa kwa uumbaji; Mungu alitamka neno kwa kiumbe kilichoumbwa na kwa kupitia hilo neno hicho kilichoumbwa mbaraka uliamriwa kwake. Kwa maana hiyo tunaona mbaraka siyo vitu bali ni neno la amri lililotamkwa ambalo mara zote hukutangulia na kuandaa mazingira kwa ajili yako. AINA ZA BARAKA • Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ...

UJUMBE WA ROHO.

 Nalikuwa katika njozi NAMI nikaona tazama watu katika mji wangu wakienndelea na shughuli zao, Lakini wanadamu wote tunaonekana tunanamchukulia MUNGU YEHOVA na IBADA ZAKE kuwa kitu Cha kawaida, inaonekana hakuna injiri ya kweli Kwa wanadamu wa muda huo. Basi ilikuwa ni siku iliyo Anza vizuri sana, Jua la ASUBUHI liliangaza vyema bila kuwepo hata wingu Moja, Ilionekana hakuna mvua inaweza kunyesha siku hiyo. Watoto walikuwa wakienndelea na michezo Yao huku watu wazima wakiendelea na shughuli zao,  GHAFRA ,. YAANI KUFUMBA NA KUFUMBUA milimani ikaonekana wingu na dhoruba Kali ambayo hapana mtu akikutwa nayo anaweza kupona, Dhoruba Kali ilikuwa inakuja mjini kwetu Kwa Kasi isiyowezekana kuikimbia. Watu wa mji walionekana wakikimbia kila mmoja aiokoe nafsi yake bila hata kuwakumbuka watoto wao na ndugu na jamaa zao. NAMI nilitaka kukimbia lakini nikawaona wanagu wadogo wakiwa wame duwaa Wanashangaa Ile tufani Kwa huzuni. Nikajiuliza inamaana hata mama Yao kwaacha? Basi nikaenda nik...

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

 JINSI YA KUMSHINDA SHETANI. sehem ya 1. Bwana Yesu asifiwe  wapendwa.   Bwana YESU amenipa wakati mzuri Mimi Jacob Wa kunieleza Na kunifunza  jinsi Na namna ya kupigana vita vya kiroho. Na ameniahidia kua kila asomaye Na atakaye nisikiliza kwanjia yoyote ile atakombolewa.  Jifunze kupigana vita vya kiroho kwa upana Mkubwa zaidi. Katika makala zangu utajifunza kushindana Na kushinda. Huwezi kushinda vita yoyote kama huna ujuzi wala mbinu za kupigana Na adui. Pia lazimaujue mbinu za adui unaye pigana naye, aina ya silaha anazo tumia, nguvu ya jeshi lake Na niwakati gani adui huwa anashambulia.  Nijambo la ajabu sana watakatifu Wa Mungu wao humchukulia shetani kama kitu cha kupuuza tena kinyonge Na kisichokua Na uwezo wala maarifa. NISAWA LAKINI NIHATARI SANA KWA UPANDE MWINGINE.  Mtu Wa Mungu elewa kwanza unapigana Na shetani ambaye Alisha hukumiwa. Hana nafasi tena ya kutubu. Tena unapigana Na shetani ambaye amepewa ulimwengu huu, anaitwa mkuu Wa Giza ...

NGUVU

 NGUVU. 1Yohana 5:4-6 “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.” Neno lolote niwafundishalo siyo mapenzi yangu bali ni mapenzi yake BABA wa Mbinguni. Mtu akiwa na NGUVU USHINDI ni wa kwake, mfano; kwenye eneo la mapambano yeyote mwenye NGUVU kuliko mwingine ndiye atakaye kuwa mshindi; au kwa wanariadha yeye mw...

WANAWAKE KUWA WACHUNGAJI

  Mistari muhimu ya kukumbuka:- 1 WAKORINTHO 14:34-36:- 34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. 35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. 36 Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu? 1 TIMOTHEO 2:11-12:- 11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. 12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Katika sehemu ya kwanza ya somo hili lilopita tuliona na kuchambua juu ya hoja potofu zinazotumiwa na watu kuhusu mwanamke kutokuwa Mchungaji au Muhubiri. Tulijiona usahihi wake na kujifunza mengi juu ya suala hilo katika kipengele hicho. Lakini leo tunamalizia juu ya hoja yao nyingine potofu na kupiga hatua tena kumalizia vile vipengele vilivyosalia. HOJA YAO YA TATU . Watasema, Katika wale mitume 12 wa Yssu . Hatuoni mahali popote ambapo Yesu alic...