Machapisho

Simba 0 Yanga 1: Yanga yailambisha Simba sakafu na kutibua sherehe za ubingwa

Picha
  Simba 0 Yanga 1: Yanga yailambisha Simba sakafu na kutibua sherehe za ubingwa  Julai 3, 2021 CHANZO CHA PICHA, YANGA SPORTS CLUB Klabu ya Yanga imewachapa watani wao wa jadi Simba SC na kuizuia klabu hiyo kutangazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania kwa msimu wa 2020/2021. Mabingwa watetezi Simba walihitaji kupata alama tatu ili kutawazwa mabingwa kwa msimu wa nne mfululizo. Hata hivyo goli la dakika ya 13 lililofungwa na Zawadi Mauya liliitosha Yanga kuifunga mdomo Simba na kulinda hadhi yake. Laiti Yanga ingelifungwa, maana yake watani wao wangetangazwa mabingwa kupitia mgongo wao. Hata hivyo licha ya kufungwa bado Simba wapo katika nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa. Simba sasa inahitaji kushinda michezo miwili kati ya minne aliyosalia nayo ili kuchukua ubingwa. Hata hivyo, ubingwa huo utakosa kionjjo muhimu cha kumfunga Yanga katika mechi zote mbili za msimu huu. Mechi ya raundi ya kwanza Simba na Yanga zilitoka sare ya goli 1-1. Katika mchezo wa leo Yanga ilitawala kipindi...

Unayajua matokeo ya kushangaza zaidi kwenye historia ya mashindano haya?

Picha
  Euro 2020: Unayajua matokeo ya kushangaza zaidi kwenye historia ya mashindano haya? julai 5,  2021 CHANZO CHA PI Tangu kuanzishwa kwake miaka zaidi ya 60 iliyopita, Michuano ya Euro imekuwa na matokeo yasiyotabirika na ya kushangaza, kuanzia ubingwa walioupata Denmark na Ugiriki mpaka ushujaa usiotarajiwa wa Iceland. BBC inakuletea matokeo 10 ya kushangaza katika historia ya michuano hiyo, ambapo matokeo ya hivi karibuni kabisa ni ya kwenye mashindano ya Euro 2016. Katika mashindano ya mwaka 2016 ambapo timu zilizoonekana kama vibonde zilizoa karibu asilimia 29 ya mechi zote zilizozaa ushindi, ikiwemo ushindi iliyoupata Ureno katika mechi ya fainali dhidi ya Ufaransa. Wakati mashindano ya Euro yakienda kuanza wiki hii, kwa kushirikiana na wataalamu wa data, Gracenote tunakueletea kumbukubu za kushangaza za mashindano haya yenye umaarufu mkubwa duniani na kushirikisha wachezaji wakubwa wa soka duniani. 10. England 0-1 Yugoslavia - (Nusu fainali - Euro 1968) Wakitoka kutwaa ub...

nyota hawa 10 wa kandanda wanapigiwa upatu kutamba Ulaya

Picha
  EURO 2020:nyota hawa 10 wa kandanda wanapigiwa upatu kutamba Ulaya julai 5, 2021 CHANZO CHA PICHA, Maelezo ya picha, Kutoka juu kushoto: Jeremy Doku, Eljif Elmas, Orkun Kokcu, Becir Omeragic, Jamal Musiala na Alexander Isak, ni miongoni mwa nyota wa kuchungwa katika michuano ya Euro 2020 Kwa sasa dunia inasubiri kwa hamu kuona kizazi kipya cha nyota wa soka, baada ya kizazi cha sasa kinachoongozwa na Cristiano Ronaldo na Leonel Messi, kuelekea mwishoni. Ukiacha kombe la dunia, ligi ya mabingwa ulaya ama ligi tano bora kubwa Ulaya, michuano mikubwa mingine inayozalisha nyota wengi wapya ni michuano ya Euro, ambayo kwa mwaka huu inaanza Ijumaa hii katika majiji 11 barani Ulaya. Michuano hii inashirikisha nyota 622 waliothibitishwa, wapo nyota wazoefu kama kina Ronaldo, Paul Pogba, Romelu Lukaku, Robert Lewandowski, Ng'olo Kante na Gareth Bale, lakini wapo pia nyota wakali wengine vijana ambao wameibuka hivi karibuni kama Kylian Mbappe wa Ufaransa, Pedri wa Hispania, Phil Foden wa E...