Machapisho

MAAMBUKIZI YA SIKIO KWA WATOTO

Picha
  MAAMBUKIZI YA SIKIO KWA WATOTO July 8, 2021 M AAMBUKIZI   au Infection ya masikio ni tatizo kubwa kwa watoto, sikio limejigawa sehemu kuu tatu ya ndani, nje na kati.    Matatizo mara nyingi yanashambulia sehemu ya kati ya sikio (Otitis media) inashambulia watoto wachanga na watoto wadogo na nyingine ni sehemu ya ndani ya sikio (Otitis externa). Hii inawashambulia sana wale wanaoogelea mara kwa mara na pia linajitokeza kipindi cha baridi. Inakuwa ngumu mzazi kujua chanzo chake, kuna baadhi ya wazazi wanadharau kufuatilia tiba yake, mwishowe masikio ya mtoto hutoa usaha mzito na harufu kali na kumpelekea kuwa na tatizo la kutokusikia vizuri. Hili tatizo linawashambulia sana watoto walio chini ya mwaka mmoja kwa asilimia 50, watoto walio na miaka mitatu na kuendelea kwa 70 na kwa watu wazima ni kwa asilimia 30. Husababishwa na bakteria au virusi wanaoshambulia kwenye ngoma ya sikio (ear drum). Kuna sababu tofauti zinazochangia mtoto kupata infection ya sikio baada ya ...

MIAMBA YA SOKA TZ sasa Yasubiriana Kigoma

Picha
  MIAMBA YA SOKA TZ sasa Yasubiriana Kigoma JULai 06 2021         BAADA ya Yanga juzi kuilaza Simba bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, mashabiki wa timu hizo jijini hapa wamesema watakutana Julai 25 huko Kigoma na mbabe atajulikana zaidi msimu huu. Katika mchezo wa juzi uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, Yanga iliichapa Simba na kufikisha pointi 70, ikiachwa alama tatu na wapinzani hao, huku ikiwa mbele kwa mechi mbili. Simba waliingia uwanjani wakihitaji ushindi ili kutangazwa mabingwa lakini Yanga walikuwa makini kuharibu mipango na kufanikiwa kupata bao mapema kupitia Zawadi Mauya na kufanya ligi kuendelea kuchangamka upande wa ubingwa. Baada ya mchezo huo wa ligi, timu hizo zinatarajia kukutana katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) utakaopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma. Sebastian Mwandala ambaye ni shabiki wa Yanga alisema timu yao haiwezi kufungwa na Simba na kwamba hizo ni salamu kuelek...

mtanikuta Kigoma MZEE MPILI

Picha
mtanikuta Kigoma MZEE MPILI JULai 06 2021         SIMBA wanalia wakiwaambia wababe wao Yanga kwamba mumshukuru Mzee wenu Mpili vinginevyo mngekula nyingi lakini mwenyewe amejibu mapigo akiwaambia ‘Hapo mmepigwa na nyuklia moja tu mmesambaratika sasa subirini Kigoma mi natangulia’. Yanga ilicheza kwa mbinu bora zaidi dhidi ya Simba juzi na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 la mapema dakika ya 11 tu kutoka kwa kiungo Zawadi Mauya na kuwacheleweshea Wekundu hao sherehe za ubingwa wa nne mfululizo. Akizungumza jana na Mwanaspoti, Mzee Mpili ambaye ni shabiki wa Yanga kutoka Ikwiriri, Pwani alisema watani wao wana bahati kwani walikuwa wapigwe nyingi katika mchezo wa juzi. Mzee Mpili ambaye alionekana kuwa mwenye furaha akiwa amevaa fulana yake safi akaenda mbali akisema safari ya kuipiga Simba ndio imeanza na sasa anatangulia mkoani Kigoma kuanza maandalizi ya mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) utakaochezwa Julai 25 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika. “Sim...

Magonjwa ya macho

Picha
  Magonjwa ya macho Jicho lenye conjunctivitis kutokana na virusi . Magonjwa ya Macho ni maradhi mbalimbali yanayoweza kuyapata macho . Jicho ni kiungo kimojawapo cha mwili kinachomsaidia mwanadamu na pia wanyama kuona vitu mbalimbali katika dunia na hata ulimwengu kwa jumla. Mnyama yeyote akikosa macho ni adhabu kubwa sana kwa maisha yake ambapo asipokuwa na mwangalizi anaweza kupata adha mbalimbali kama kukosa chakula na inaweza kumpelekea mnyama kufa kwa kukosa chakula kwa sababu haoni. Magonjwa ya macho yapo ya aina mbalimbali: mengine yanasababishwa na nzi , kama vile trakoma , na mengine yanasababishwa na mionzi ambayo inaweza kuwa ya jua , runinga na hata tarakilishi ambavyo vinasababisha macho kutofanya kazi vizuri kama kuona mbali na kuona karibu na pia kichwa kuuma . Makengesa katika macho yanasababishwa na kulegea kwa mishipa ya siliari inayoshika lenzi ya jicho. Magonjwa yote ya macho yanatibika; inategemea hatua ya ugonjwa huo wa macho ulipof...

Siku 100 za Rais Samia Suluhu: Kibarua kilichopo mbele serikali ya kudhibiti corona

Picha
  Siku 100 za Rais Samia Suluhu: Kibarua kilichopo mbele serikali ya kudhibiti corona 05julai  2021  picha, Ikulu, Tanzania Maelezo ya picha, Rais Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya kamati maalum ya corona kutoka kwa Profesa Said Aboud. Ripoti iliyozinduliwa na kamati maalum ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhusu COVID-19, bila shaka imeiweka nchi hiyo katika ramani ya dunia kuhusu maswala ya usalama wa afya ulimwenguni. Hata hivyo, kwa kuzingatia hali ilivyo kwa sasa nchini humo, serikali inakabiliwa na jukumu zito la kutekeleza kikamilifu mapendekezo ya wanasayansi. Changamoto iliyowazi kwa sasa ni kuwepo kwa mkanganyiko mkubwa kijamii na kisaikolojia uliochagizwa na utata wa mbinu zilizotumika dhidi janga la COVID-19 wakati wa utawala wa hayati Rais John Magufuli. Tofauti na ilivyo sasa, ukweli uko kwenye rekodi kwamba utawala uliopita haukuwa wazi kuhusu kuwepo kwa janga nchini licha ya viongozi wa dini na wanaharakati kupaza sauti juu ya uwepo ...

Katiba Mpya Tanzania: Ni mtego kwa Rais Samia?

Picha
  Katiba Mpya Tanzania: Ni mtego kwa Rais Samia? July 1 2021 CHANZO CHA PICHA, jaco online tv Maelezo ya picha, Jaji Warioba Safari ya mchakato wa kupata katiba mpya ya Tanzania ulianza tangu mwaka 2010, wakati Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete alipoamua kuutangazia umma dhamira na nia ya serikali ya kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya. Mchakato ukaanza rasmi mwaka 2011 kwa kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Na. 83/2011 na baadaye ikatungwa Sheria nyingine ya Kura ya Maoni Na. 11/2013. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilitamka kuanzishwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilianzishwa chini ya Waziri mkuu wa zamani, Jaji Joseph Sinde Warioba, ikaratibu mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa rasimu ya kwanza ya katiba ambayo kupitia uhariri wa Mabaraza ya Katiba ikapatikana Rasimu ya Pili ya Katiba. Je, mabadiliko ya kisiasa 'kutoyumbishwa' tena Tanzania? Rasimu hii ya pili ambayo ni maarufu kama Rasimu ya Warioba ikawasilishwa kwenye Bu...