Machapisho

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 13.07.2021

Picha
  Manchester United wako mbioni kukubaliana masharti binafsi na mlinzi wa Real Madrid Raphael Varane,27, ambaye amekuwa akitolewa macho kwa muda mrefu.(Daily Mail) Hector Bellerin ameiambia Arsenal kuwa anataka kuondoka wakati wa dirisha la usajili majira ya joto. Mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi mwenye miaka 26, ambaye ni mchezaji wa muda mrefu wa kikosi cha kwanza cha Mikel Arteta ana matumaini ya kuhamia Inter Milan. (Metro) Manchester City haina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Mfaransa Antoine Griezmann, 30, lakini wana nia na mshambuliaji wa Norway na Borussia Dotmund Erling Braut Haaland, 20, na nahodha wa Tottenham England Harry Kane. (The Sun) Chelsea inatarajia kutangaza 'ofa kubwa' kwa Haaland. (Daily Star) Griezman anaweza kuelekea kwenye klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid, kwa kubadilishana na kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez,26. (Daily Express) Tweet ya kiungo wa kati wa Real Madrid Isco -iliyofutwa - inadokeza kwamba mch...

Katiba ya sasa inatoa nafuu kwa CCM?

Picha
 Mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya nchini Tanzania ulianza rasmi mwaka 2011 wakati wa utawala wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete. Miaka mitatu baadaye yaani mwaka 2014, wakati huo Kikwete akimalizia muda wake madarakani mchakato huo ulikwama ukiwa katika hatua ya mwisho ya upigaji kura wa katiba inayopendekezwa. Wengi walidhani baada ya kuingia madarakani John Pombe Magufuli, mchakato huu ungepewa kipaumbele lakini mbele ya waandishi wa habari alieleza katiba mpya haikuwa kipaumbele cha utawala wake. Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 - 2020, iliiweka hoja ya kuendelea na mchakato wa kupata katiba mpya. Baadaye hoja hiyo iliondolewa katika ilani iliyofuata. Na haikuwa tena kipau mbele kwa chama hicho. Kutoka wakati huo hadi sasa kuna upinzani kuhusu kuendeleza gurudumu la katiba mpya kutoka CCM. Mchakato wa katiba umegeuzwa danadana kuanzia mwendazake Magufuli na Rais wa sasa Samia Suluhu Hasssan. Kutoka kuwa jambo lililoachisha watu shughuli zao kul...

chanzo cha moto Kariakoo Kuchunguzwa

Picha
    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atembelea soko la Kariakoo kushuhudia hasara iliyosababishwa na moto. Picha kwa hisani ya Global Publishers TV, Dar es Salaam, Tanzania. Kufuatia kuungua moto Soko la kimatiafa la Kariakoo Jijini Dar es salaam, nchini Tanzania, Serikali imeunda tume kuchunguza chanzo cha moto huo ulioteketeza maduka zaidi ya mia nne yalioko katika jengo la Soko hilo maarufu. Viongozi mbalimbali wametembelea eneo hilo wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ambaye ameagiza uchunguzi huo kufanyika ndani ya siku saba. Pia Majaliwa ameahidi kuwa serikali itazungumza na mabenki yaliyo wakopesha Wafanyabiashara waliounguliwa na maduka yao. Aidha changamoto ya vifaa kwa Idara ya Zimamoto pamoja na miundombunu hafifu katika eneo hilo vinaelezwa kuchangia pakubwa athari zaidi za moto huo ulioanza kuwaka majira ya saa moja jioni Jumamosi tarehe 10 na kuteketeza maduka na mali za wafanyabiashara katika soko hilo. Tathmini halisi ya hasara iliyosababisha na ...

Soko Kuu Mombasa lateketea kwa moto

Picha
  Soko maarufu la Marikiti mjini Mombasa nchini Kenya limepata hasara kubwa kutokana na moto ambao ulilikumba soko hilo Jumamosi usiku kuamkia Jumapili. Wafanya biashara katika soko maarufu la Marikiti mjini Mombasa wamepata hasara kubwa baada ya moto mkubwa kushuhudiwa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili Hakuna ripoti za maafa wala majeruhi kufikia sasa huku juhudi za kuzima moto huo zikiendelea. Magari ya zima moto kutoka kitengo cha serikali za ugatuzi wakishirikiana na polisi wako kwenye tukio wakijaribu kudhibiti hali. Wakati huu ambapo kuna sharti la kutotoka nje wakati wa usiku kwa sababu ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona, baadhi ya wakaazi wa maeneo ya karibu wako nje kushuhudia moto huo na wengine wakitoa msaada wa kudhibiti moto. Hali hii imewalazimu maafisa wa kushika doria nyakati hizo kuweka usalama eneo hilo pia kuepusha visa vya uporaji kutokea kwenye baadhi ya maduka yaliyoachwa wazi kutokana na moto huo. Haijabainika chanzo cha moto huo, na hakuna mwenye kuf...

timu ya kiufundi yatumwa nchini haiti kutoka MAREKANI

Picha
                              Rais wa Haiti aliyeuwawa Jovenel Moise kwenye picha ya awali. (wa pili kutoka kushoto) Marekani Jumapili imetuma timu ya kiufundi nchini Haiti kutathmini hali ya usalama na mahitaji mengine baada ya mauaji ya rais Jovenel Moise wiki iliyopita. Haikuelezwa wazi ni taasisi zipi zimeshirikishwa, lakini timu hiyo inapanga kuwasilisha ripoti kwa rais Joe Biden itakaporudi nyumbani, kabla ya maamuzi kuchukuliwa juu ya kuhusika zaidi kwa Marekani katika mzozo mbaya unaokikumba kisiwa hicho cha Caribbean, afisa mwandamizi ameambia shirika la habari la Reuters. Awali, Marekani ilitupilia mbali ombi la Haiti la kuitaka kusaidia kuzima ghasia zilizofuatia kuuwawa kwa rais Moise Jumatano. Kiongozi huyo aliuwawa kwa kupigwa risasi wakati akiwa nyumbani kwake, kwenye mji mkuu wa Port au Prince. Idara ya polisi nchini humo imesema kuwa wamarekani wawili na wacolombia 26 baadhi yao wakiwa wanajeshi ...

aua mtoto wake kisa covid 19

Picha
  Raia mmoja katika Wilaya ya Kalaki nchini Uganda (35), anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumnyonga hadi kufa mwanaye mwenye umri wa miezi tisa baada ya kukosa kupokea msaada wa Sh 100,000 kwa watu wasiojiweza wa kujikidhi katika kipindi cha tahadhari ya corona. Hivi karibuni serikali ya nchi hiyo iliahidi kutoa Sh 100,000 kwa watu wasiojiweza ili kuweza kujikimu kwa kipindi cha siku 42 ambacho walipaswa kukaa ndani ikiwa ni moja ya hatua za kujikinga na maambukizi ya corona. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa wilaya hiyo, Paul Kalikwani mtuhumiwa aliposikia baadhi ya watu wamepokea kiasi hicho cha fedha kwenye simu zao lakini kwake hakuwa amepata ujumbe wowote aliamua kufanya maamuzi hayo ya kumyonga mtoto wake. Awali mtuhumiwa huyo alishawahi kusikika akiwaambia wanakijiji wenzake kuwa iwapo serikali haitampatia fedha hizo ataua familia yake yote.

Chanjo ya Oxford / AstraZeneca COVID-19: unachohitaji kujua

Picha
Chanjo ya Oxford / AstraZeneca COVID-19: unachohitaji kujua   ukweli kwamba WHO imeorodhesha matoleo mawili ya chanjo ya AstraZeneca / Oxford COVID-19 kwa matumizi ya dharura. Ili kuonyesha Kamati ya Ushauri ya hivi karibuni ya WHO juu ya taarifa ya Usalama wa Chanjo. Kikundi cha Wataalam wa Kimkakati cha Ushauri wa Chanjo (SAGE) kimetoa mapendekezo ya muda kwa matumizi ya chanjo ya Oxford / AstraZeneca COVID-19 (AZD1222).   Nani anapaswa kupewa chanjo kwanza?   Wakati usambazaji wa chanjo ni mdogo, inashauriwa kuwa kipaumbele kitolewe kwa wafanyikazi wa afya walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa na watu wazee, pamoja na wale walio na umri wa miaka 65 au zaidi. Nchi zinaweza kutaja Miongozo ya Njia ya Kipaumbele cha WHO na Mfumo wa Maadili wa WHO kama mwongozo wa upendeleo wao kwa vikundi lengwa.   Ni nani mwingine anayeweza kuchukua chanjo?   Chanjo inapendekezwa kwa watu walio na ugonjwa ambao umetambuliwa kama unaongeza hatari ya ...