KUONGOZWA NA ROHO.

KUONGOZWA NA ROHO. Maombi ni lazima, tumehimizwa na muumbaji kuomba, Kwa kila mwamini anapaswa kuwa na mambo yafuatayo:- 1. Afanye kazi, 2. Awe na umiliki juu ya nchi, 3. Azalishe, 4. Aombe, 5. Ashuhudie, 6. Aabudu, 7. Lazima awe mtoaji, 8. Lazima uwe na upendo, penda uumbaji, 9. Lazima asamehe na atubu, 10. Ahakikishe anatunza wito wake. Ukiyaweka haya pamoja ndipo unakuwa yule ambaye Mungu anampenda, 1 Wakorintho 2:10 “ Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. ” Mungu ametupa ufunuo kupitia roho wake, ufunuo ni nini? Maana yake ni kugundua mambo yaliyo sirini, maswala ya kiroho ukiyagundua yale yanayo kuhusu wewe, Mungu au ya i...