Machapisho

Ukombozi na Uponyaji.

Picha
   Ukombozi na Uponyaji.   Paulo na sila walifungiwa mahali kwa sababu mapepo waliamua kumtumia mfalme ili kuliharibu kanisa, waliwafungia mahali wakifikiri kuwa sauti zao hazitasikiwa, lakini ilipofika usiku Paulo na Sila wakaamua kuimba na walipoimba Mbingu ilishangaa na kuja kuwasaidia. Kuna miujiza itatokea ambayo haujawahi kuiona, inaweza ikawa unataarifa mbaya kutoka kwa madaktari kuwa kutokana na ugonjwa ulionao inapaswa utolewe kizazi na hautaweza kuzaa tena, au umeambiwa ugonjwa ulionao hauna dawa, na wengine wameambiwa kuwa ugonjwa ulio nao utakuwa nao mpaka ufe, sikia nikwambie ni hivi ibilisi ndio atakayekufa na huo ugonjwa lakini si wewe, Yesu alikufa msalabani kwa ajili yako. Unaweza ukawa katika ukoo wenu hakuna aliyewahi kuendesha gari na wewe na kaka zako na mabinamu zako hakuna anaye endesha gari kwa sababu mmefungiwa mahali, lakini leo utatoka kwa Jina la Yesu. Yesu hakwenda msalabani kwa ajili yake mwenyewe, bali alikwenda kwa ajili yako, siku ...

Mungu akitokea kwako kama mfalme ana sehemu zake nne.

Picha
  Mungu akitokea kwako kama mfalme ana sehemu zake nne. 1. Mshauri, Ukifikia hatua hii ndiyo wakati huu kitu cha kwako kinakuwa cha kwake na cha kwake kinakuwa cha kwako. Hivyo huwezi kukubali kuona Matakatifu ya Mungu yanachafuliwa ndivyo hasira ya Mungu inawaka juu yako, kuna watu wanakasirika wakisengenywa wao lakini wachungaji au viongozi wao akisengenywa unaona kawaida, jifunze kuyalinda matakatifu ya Mungu hata kama yatakughalimu.  Mungu ana njia nyingi za kuwapa watu wake unatakiwa uwe na wivu wa Mungu.   2. Mungu mwenye nguvu, Lengo lakujionyesha ni kukufanya uweze kufika kwenye kufanya miujiza na pia kupokea miujiza na pia uweze kufanya yale ambayo ulikuwa huwezi kufanya ana maana gani? Anamaanisha atakupa usaidizi kwa sababu wewe ni raia wake.   3. Baba wa milele, ili kukupa wewe urithi wako, kukufanya urithi, yamkini baba yako hana chochote au alishakufa, unachotakiwa kujua yupo Baba wa mbinguni ambaye Yeye atakupa urithi wako. neno baba maana yake n...

KUFIKIA MATARAJIO YAKO.

Picha
  KUFIKIA MATARAJIO YAKO. Tupo katika mchakato wa kuyaendea mafanikio yako na matarajio yako. Tukiangalia safari ya wana wa Israel inatupa maswali mengi ya kujiuliza kwa maana Biblia inasema safari yao ni kivuli cha safari yetu katika wokovu, ukitaka kujua safari yako ikoje na inaishiaje angalia safari ya wana wa Israel, itakupa mwangaza wa safari unayoiendea. Ninapo itazama safari ya wana wa Israel nina maswali, je! Ni wangapi watakao faulu kufika mwisho wa safari yao? Wana wa Israel walikuwa wanaenda katika nchi ya dhahabu, maziwa na asali, hawakuwa na safari ya kwenda mbinguni bali ni safari ya kuendea matarajio na mbaraka wao. Kama kuna wakati wa kujiuliza maswali ni kupitia safari ya wana wa Israel ambayo kwetu sisi ndio kioo na ramani yetu ya kuelekea uzima wa milele. Kabla haujaanza safari yako ya kuelekea katika Baraka zako ziko changamoto nyingi utakutana nazo kama vile wana wa Israel walivyokutana nazo walivyokuwa njiani, hayo yaliyowasibu na wewe ukubali au usikuba...

INJILI NA MAZINGIRA YA MTU.

Picha
  INJILI NA MAZINGIRA YA MTU. Wafilipi 3:7-8 “ Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo ;”   Paulo alikuwa mwaminifu katika dini yake ya Kiyahudi aliyokuwa nayo, Bwana akamgeuza na kumuingiza upande wa pili yaani upande wa Yesu ili aweze kufanya vizuri upande huu; tunamuona Paulo hata alipoingia upande wa Yesu alisimama na kuihubiri injili kwa uaminifu, kuna watu ambao wana roho au tabia ya uaminifu ndani yao hata kabla hawajaokoka, Mungu wa Mbinguni anamgeuza huyo mtu ili apate kumwabudu Mungu wa kweli na kutenda vizuri na kwa uaminifu wote. Unaweza kumkuta mtu anatamani kusonga mbele lakini kuna watu wanamzuia asisonge mbele, unapaswa kuwa mwaminifu ili Mungu asimame na wewe na kukupa wepesi wakusonga mb...