Machapisho

Kwa Wewe ambaye bado hujaolewa,

  Kwa Wewe ambaye bado hujaolewa, usitafute kuolewa na Malaika (mwanaume asiye na mapungufu) hutakaa umuone hata mmoja, mimi nawafahamu wanaume, mwanangu hutakaa umpate asiye na udhaifu (mapungufu) lakini kabla hujaolewa angalia hicho kichwa kinachokuoa kikoje? Angalia AKILI yake na usiangalie leo ana nini, inawezekana hana pesa nyingi leo lakini kama ana AKILI pesa zitakuja.   Elewa yule anayekuoa ana udhaifu na Mungu anakupeleka kwake ili ukaushughulikie. Hakuna udhaifu usioleta aibu bali ukiuona udhibiti. Mwingine udhaifu wake ni hasira anapiga watu au hata wewe anakupiga, ukiona hivyo usibebe vitu ukakimbia bali kumbuka umepelekwa pale ili kudhibiti huo udhaifu.   Mwanaume yeyote anayempiga mke wake ni mpumbavu na ili kuondoa huo upumbavu wewe kama mke jifunze kumsifia, mwambie namshukuru Mungu kwa kunipa mume kama wewe, sifa zinaondoa ujinga.   Mwambie Mungu akutie Nguvu ili upate kushinda na sio kukimbilia kudai taraka kwa maana Mungu anachukia kuachana .

MATUMIZI YAKO

  Jitahidi matumizi yako yalingane na mapato yako wala yasivuke kiwango kinachotakiwa vinginevyo utakuwa na madeni au utaiba na mwivi ni mzigo kwa wengine. Angalia matumizi yako yasiingilie akiba yako ukashindwa kufika ulikokusudiwa. Usiige maisha ya watu wengine au kujiweka daraja la juu kwa kuombaomba, huo ni upumbavu, bali ishi katika daraja lako. Jipime unatumiaje muda, fursa, nguvu na mapato yako. Kwa nini uishi nyumba usiyomudu wakati uwezo wako ni mdogo? Ishi kwenye nyumba yako hata kama siyo ya bati maana Mungu anatukuzwa kwa kilicho chako. Waamini wana tatizo la kupenda vitu vya bure, ni kosa kubwa kupanga nyumba ya mtu bila kulipa. Wokovu ni bure, lakini siyo rahisi, una gharama na Yesu alikufa kwa ajili hiyo. Mtakatifu kama hana fedha, anaweza kusahau kama ameokoka; kwa hiyo pambanua mambo ya siku zote na yale maalumu ili ujue kipi cha kufanya kwanza. Walawi 10: 8-10 "Kisha BWANA akanena na Haruni, na kumwambia, usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoj...

MWANA MPOTEVU.

Picha
  MWANA MPOTEVU. Luka 15:11-32 “ Akasema, Mtu Mmoja Alikuwa Na Wana Wawili; Yule Mdogo Akamwambia Babaye, Baba, Nipe Sehemu Ya Mali Inayoniangukia. Akawagawia Vitu Vyake. Hata Baada Ya Siku Si Nyingi, Yule Mdogo Akakusanya Vyote, Akasafiri Kwenda Nchi Ya Mbali; Akatapanya Mali Zake Huko Kwa Maisha Ya Uasherati…….. ” Mwana Mpotevu Alichukua Sehemu Ya Mali Inayomuangukia Na Kuondoka Nayo Lakini Pia Alidhani Akiondoka Na Hiyo Mali Atakenda Kufanikiwa, Baba Yake Alipompa Hiyo Mali Alikuwa Na Tumaini Kuwa Atazalisha Na Kupata Faida, Lakini Ikawa Ni Kinyume Chake Kwa Maana Aliitapanya Hiyo Mali Na Akaishia Kula Na Nguruwe. Maisha Ya Mwana Mpotevu, Hakujali Ubaadae Wa Kesho Yake, Bali Alichojali Ni Kile Alichokipata Na Kukitumia. Mwana Mpotevu Aliijua Nafasi Aliyonayo Kwa Baba Yake Na Ndio Maana Akaenda Na Kudai Haki Yake. Sifa Za Mwana Mpotevu: 1. Alikuwa Ni Mtu Wa Kuzingatia, Alijua Kwa Baba Yake Kuna Kila Kitu Na Yeye Ni Sehemu Ya Hiyo Mali, Akilini Mwake Alijua Kuwa Lazima Ach...
Picha
  Historia ya Wokovu Jinsi Pietro Perugino alivyochora Mateso ya Yesu msalabani kwa mtindo wa Stabat Mater , yaani akiwa na Bikira Maria na Mtume Yohane chini yake ( 1482 ). Kifo na ufufuko wa Yesu ndiyo kilele cha historia ya wokovu kwa imani ya Ukristo . Kwa jina hilo Wakristo wanamaanisha ufafanuzi wa mpango wa kazi ya Mungu kwa wokovu wa binadamu kadiri ya Biblia . Yaliyomo 1 Maana ya historia 2 Maana ya wokovu 3 Imani kuhusu Biblia 4 Agano la Kale 4.1 Vitabu vitano vya Torati 4.2 Uumbaji 4.3 Dhambi ya asili 4.4 Watu walivyoishi baada ya dhambi 4.5 Nuhu 4.6 Mnara wa Babeli 4.7 Abrahamu (1900-1800 hivi K.K.) 4.8 Watoto wa Isaka: Esau na Yakobo 4.9 Yosefu na ndugu zake kushukia Misri (1700 hivi K.K.) 4.10 Utumwa wa Misri na wito wa Musa (1250 hivi K.K.) 4.11 Mapigo ya Wamisri 4.12 Safari ya kuendea Nchi ya ahadi 4.13 Agano la Mlima Sinai 4.14 Ndama ya dhahabu 4.15 Mungu kujifunua ten...