Machapisho

WAABUDUO

Picha
SOMO: WAABUDUO     Mwanzo 1:1-2 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.” Hapo mwanzo tunamuona Mungu akiumba mbingu na nchi, yapasa tufahamu nadharia yetu ya ibada, nadharia yetu ni nini? Ni mwanzo, tukiufahamu mwanzo basi tunaweza kuabudu katika uhalisia wa Ibada. Biblia inasema hapo mwanzo Mungu, si Efatha, Josephat wala waabuduo bali hapo mwanzo tunamuona Mungu akifanya kazi ya uumbaji. Alichokiumba kilikuwa ni kitupu na kikiwa, hii inamaana kuwa hicho alichokiumba Mungu kilikuwa kinahitaji utimilifu. Mwanzo 1:3 “ Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.” Hapa tunagundua ibada ni Nuru, hii inamaana gani? Utimilifu, na ukamilifu ni mzuri. Tunapoabudu yapasa tuanze mwanzo na tu...

Tunamamlaka yote ya kuziharibu kazi za ibilisi,

Picha
   Ukombozi na Uponyaji.   Paulo na sila walifungiwa mahali kwa sababu mapepo waliamua kumtumia mfalme ili kuliharibu kanisa, waliwafungia mahali wakifikiri kuwa sauti zao hazitasikiwa, lakini ilipofika usiku Paulo na Sila wakaamua kuimba na walipoimba Mbingu ilishangaa na kuja kuwasaidia. Kuna miujiza itatokea ambayo haujawahi kuiona, inaweza ikawa unataarifa mbaya kutoka kwa madaktari kuwa kutokana na ugonjwa ulionao inapaswa utolewe kizazi na hautaweza kuzaa tena, au umeambiwa ugonjwa ulionao hauna dawa, na wengine wameambiwa kuwa ugonjwa ulio nao utakuwa nao mpaka ufe, sikia nikwambie ni hivi ibilisi ndio atakayekufa na huo ugonjwa lakini si wewe, Yesu alikufa msalabani kwa ajili yako. Unaweza ukawa katika ukoo wenu hakuna aliyewahi kuendesha gari na wewe na kaka zako na mabinamu zako hakuna anaye endesha gari kwa sababu mmefungiwa mahali, lakini leo utatoka kwa Jina la Yesu. Yesu hakwenda msalabani kwa ajili yake mwenyewe, bali alikwenda kwa ajili yako, siku il...

Kwa Wewe ambaye bado hujaolewa,

  Kwa Wewe ambaye bado hujaolewa, usitafute kuolewa na Malaika (mwanaume asiye na mapungufu) hutakaa umuone hata mmoja, mimi nawafahamu wanaume, mwanangu hutakaa umpate asiye na udhaifu (mapungufu) lakini kabla hujaolewa angalia hicho kichwa kinachokuoa kikoje? Angalia AKILI yake na usiangalie leo ana nini, inawezekana hana pesa nyingi leo lakini kama ana AKILI pesa zitakuja.   Elewa yule anayekuoa ana udhaifu na Mungu anakupeleka kwake ili ukaushughulikie. Hakuna udhaifu usioleta aibu bali ukiuona udhibiti. Mwingine udhaifu wake ni hasira anapiga watu au hata wewe anakupiga, ukiona hivyo usibebe vitu ukakimbia bali kumbuka umepelekwa pale ili kudhibiti huo udhaifu.   Mwanaume yeyote anayempiga mke wake ni mpumbavu na ili kuondoa huo upumbavu wewe kama mke jifunze kumsifia, mwambie namshukuru Mungu kwa kunipa mume kama wewe, sifa zinaondoa ujinga.   Mwambie Mungu akutie Nguvu ili upate kushinda na sio kukimbilia kudai taraka kwa maana Mungu anachukia kuachana .

MATUMIZI YAKO

  Jitahidi matumizi yako yalingane na mapato yako wala yasivuke kiwango kinachotakiwa vinginevyo utakuwa na madeni au utaiba na mwivi ni mzigo kwa wengine. Angalia matumizi yako yasiingilie akiba yako ukashindwa kufika ulikokusudiwa. Usiige maisha ya watu wengine au kujiweka daraja la juu kwa kuombaomba, huo ni upumbavu, bali ishi katika daraja lako. Jipime unatumiaje muda, fursa, nguvu na mapato yako. Kwa nini uishi nyumba usiyomudu wakati uwezo wako ni mdogo? Ishi kwenye nyumba yako hata kama siyo ya bati maana Mungu anatukuzwa kwa kilicho chako. Waamini wana tatizo la kupenda vitu vya bure, ni kosa kubwa kupanga nyumba ya mtu bila kulipa. Wokovu ni bure, lakini siyo rahisi, una gharama na Yesu alikufa kwa ajili hiyo. Mtakatifu kama hana fedha, anaweza kusahau kama ameokoka; kwa hiyo pambanua mambo ya siku zote na yale maalumu ili ujue kipi cha kufanya kwanza. Walawi 10: 8-10 "Kisha BWANA akanena na Haruni, na kumwambia, usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoj...

MWANA MPOTEVU.

Picha
  MWANA MPOTEVU. Luka 15:11-32 “ Akasema, Mtu Mmoja Alikuwa Na Wana Wawili; Yule Mdogo Akamwambia Babaye, Baba, Nipe Sehemu Ya Mali Inayoniangukia. Akawagawia Vitu Vyake. Hata Baada Ya Siku Si Nyingi, Yule Mdogo Akakusanya Vyote, Akasafiri Kwenda Nchi Ya Mbali; Akatapanya Mali Zake Huko Kwa Maisha Ya Uasherati…….. ” Mwana Mpotevu Alichukua Sehemu Ya Mali Inayomuangukia Na Kuondoka Nayo Lakini Pia Alidhani Akiondoka Na Hiyo Mali Atakenda Kufanikiwa, Baba Yake Alipompa Hiyo Mali Alikuwa Na Tumaini Kuwa Atazalisha Na Kupata Faida, Lakini Ikawa Ni Kinyume Chake Kwa Maana Aliitapanya Hiyo Mali Na Akaishia Kula Na Nguruwe. Maisha Ya Mwana Mpotevu, Hakujali Ubaadae Wa Kesho Yake, Bali Alichojali Ni Kile Alichokipata Na Kukitumia. Mwana Mpotevu Aliijua Nafasi Aliyonayo Kwa Baba Yake Na Ndio Maana Akaenda Na Kudai Haki Yake. Sifa Za Mwana Mpotevu: 1. Alikuwa Ni Mtu Wa Kuzingatia, Alijua Kwa Baba Yake Kuna Kila Kitu Na Yeye Ni Sehemu Ya Hiyo Mali, Akilini Mwake Alijua Kuwa Lazima Ach...