Machapisho

UKOMBOZI NA UPONYAJI

 Ukombozi na Uponyaji. Paulo na sila walifungiwa mahali kwa sababu mapepo waliamua kumtumia mfalme ili kuliharibu kanisa, waliwafungia mahali wakifikiri kuwa sauti zao hazitasikiwa, lakini ilipofika usiku Paulo na Sila wakaamua kuimba na walipoimba Mbingu ilishangaa na kuja kuwasaidia. Kuna miujiza itatokea ambayo haujawahi kuiona, inaweza ikawa unataarifa mbaya kutoka kwa madaktari kuwa kutokana na ugonjwa ulionao inapaswa utolewe kizazi na hautaweza kuzaa tena, au umeambiwa ugonjwa ulionao hauna dawa, na wengine wameambiwa kuwa ugonjwa ulio nao utakuwa nao mpaka ufe, sikia nikwambie ni hivi ibilisi ndio atakayekufa na huo ugonjwa lakini si wewe, Yesu alikufa msalabani kwa ajili yako. Unaweza ukawa katika ukoo wenu hakuna aliyewahi kuendesha gari na wewe na kaka zako na mabinamu zako hakuna anaye endesha gari kwa sababu mmefungiwa mahali, lakini leo utatoka kwa Jina la Yesu. Yesu hakwenda msalabani kwa ajili yake mwenyewe, bali alikwenda kwa ajili yako, siku ile Yesu alimshinda ib...

KUONGOZWA NA ROHO

 KUONGOZWA NA ROHO. Maombi ni lazima, tumehimizwa na muumbaji kuomba, Kwa kila mwamini anapaswa kuwa na mambo yafuatayo:- 1.      Afanye kazi, 2.      Awe na umiliki juu ya nchi, 3.      Azalishe, 4.      Aombe, 5.      Ashuhudie, 6.      Aabudu, 7.      Lazima awe mtoaji, 8.      Lazima uwe na upendo, penda uumbaji, 9.      Lazima asamehe na atubu, 10.  Ahakikishe anatunza wito wake.   Ukiyaweka haya pamoja ndipo unakuwa yule ambaye Mungu anampenda,   1 Wakorintho 2:10 “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.” Mungu ametupa ufunuo kupitia roho wake, ufunuo ni nini? Maana yake ni kugundua mambo yaliyo sirini, maswala ya kiroho ukiyagundua yale yanayo kuhusu wewe, Mungu au ya ibilisi yaliyo katika roho hiki ndicho tunakiita ufunuo inamaana yamefunuliwa kwako. Biblia inasema “Lakini Mu...

Uzazi wa mpango kwa kutumia njia za asili

Picha
  Open main menu Uzazi wa mpango kwa njia asilia Lugha Download P Uzazi wa mpango kwa njiap asilia   maana yake ni   mbinu   zile za kuzuia   mimba   isipatikane katika   tendo la ndoa   ambazo zinafuata   maumbile   tu. Njia asilia za kupanga  uzazi  ni mbinu ambazo hazihusishi  vifaa  wala  kemikali , bali zinategemea  ufahamu  wa  uwezo  wa  mwanamke  kupata au kutopata mimba wakati wa kufanya tendo la ndoa. Wanawake ambao wananyonyesha na wanapenda kukwepa mimba wanaweza kufanya tendo la ndoa kwa kutegemea kukatizwa kwa  hedhi  wakati wa kunyonyesha. Mbali ya huo  ujuzi  wa jumla, uzazi unaweza kupangwa kwa kutofanya tendo la ndoa siku 13 hivi ambapo katika mzunguko wa hedhi kuna uwezekano wa kupata mimba. Kinyume chake wanandoa wanaweza kulenga uzazi kwa hakika zaidi wakifanya tendo la ndoa kwa kutumia vizuri siku zinazouwezesha. Vilevile wanaweza kuchagua...

WAABUDUO

Picha
SOMO: WAABUDUO     Mwanzo 1:1-2 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.” Hapo mwanzo tunamuona Mungu akiumba mbingu na nchi, yapasa tufahamu nadharia yetu ya ibada, nadharia yetu ni nini? Ni mwanzo, tukiufahamu mwanzo basi tunaweza kuabudu katika uhalisia wa Ibada. Biblia inasema hapo mwanzo Mungu, si Efatha, Josephat wala waabuduo bali hapo mwanzo tunamuona Mungu akifanya kazi ya uumbaji. Alichokiumba kilikuwa ni kitupu na kikiwa, hii inamaana kuwa hicho alichokiumba Mungu kilikuwa kinahitaji utimilifu. Mwanzo 1:3 “ Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.” Hapa tunagundua ibada ni Nuru, hii inamaana gani? Utimilifu, na ukamilifu ni mzuri. Tunapoabudu yapasa tuanze mwanzo na tu...