TBJoshua kuzikwa leo Nigeria
TBJoshua kuzikwa leo Nigeria AFP Copyright: AFP TB Joshua mara kwa mara alitembelea Afrika, Uingereza na Amerika Kusini Image caption: TB Joshua mara kwa mara alitembelea Afrika, Uingereza na Amerika Kusini Muhubiri wa Televisheni Nigeria TB Joshua anazikwa leo Ijumaa katika mji mkuu wa nchi hiyo Lagos baada ya wiki ya kutoa heshima za mwisho. Maelfu ya waombolezaji wamekusanyika katika kanisa lake la Synagogue, Church of All Nations (SCOAN) lililopo kweye eneo laIkotun mjini Lagos. Marehemu Joshua aliyekuwa na umri wa miaka 57 alifariki tarehe 5 Juni baada ya kuugua kwa muda mfupi, kulingana na kanisa. Temitope Balogun Joshua aliheshimiwa na watu kutoka kote duniani na makumi ya maelfu ya watu walihudhuria ibada zake kila wiki. Kupanda kwa umaarufu wake katika miaka ya 1990 kuliambatana na vipindi vya " miujiza" vilivyooneshwa kwenye televisheni za Nigeria na wachungaji. Mafundisho yake yalitabiri uponyaji wa kila aina wa magonjwa, ikiwa ni pamoja na HIV/Ukimwi na aliwav...