Nini maana ya kufunga?

Isaya 58:6-14 “ Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde……. ” · Kufunga maana yake ni kuachilia matendo maovu. · Kufunga ni kukusababisha wewe kutimiza mapenzi ya Muumba wako, · Kufunga ni kumwambia Mungu mimi sistahili pasipo wewe, yaani inamaana ni kumkaribia Mungu. · Kufunga ni kuuita uwepo wa Mungu uwe pamoja nawe na kutembea na wewe, uwepo wa...