Machapisho
Nini maana ya kufunga?
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine

Isaya 58:6-14 “ Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde……. ” · Kufunga maana yake ni kuachilia matendo maovu. · Kufunga ni kukusababisha wewe kutimiza mapenzi ya Muumba wako, · Kufunga ni kumwambia Mungu mimi sistahili pasipo wewe, yaani inamaana ni kumkaribia Mungu. · Kufunga ni kuuita uwepo wa Mungu uwe pamoja nawe na kutembea na wewe, uwepo wa...
Agano la kale na Agano jipya
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine

Mungu alifanya Agano mara mbili, • Agano la Kale; Agano hili ni Agano la siku ambayo Mungu aliagana na Musa. • Agano Jipya; Agano hili ni la Damu ambalo Mungu alilifanya na Yesu. Lakini Biblia inasema Utukufu wa mwisho utakuwa mkubwa kuliko ule wa kwanza. Malango ya kuzimu yalikuwa na nguvu juu ya Agano la siku yaani Agano la Kale, Agano la Kwanza lilitembea katika laana lakini Agano la Pili lilitembea katika Nguvu ya Mungu hivyo malango ya kuzimu hayana nguvu ya kulishinda. Agano la Kwanza mtu alikuwa akiwa na mapepo anapigwa mawe mpaka afe, lakini Agano Jipya mtu akiwa na pepo anaombewa na huyo pepo anatoka. Agano la Kwanza lilikuwa katika siku lakini Agano la Pili hakuna Agano juu ya siku bali tunakumbuka yale yaliyotokea (matukio), hii ina maana kuwa tulihama kutoka katika siku na kuwa katika tendo. Baada ya kuhama kutoka katika siku na kuingia katika tendo, hii ndiyo lilikuwa ni kumhalalisha mtu kuwa bwana wa siku yake, tendo hilo lilimuondoa mtu kutoka katika ...
Kwa nini tunasifu kama sehemu ya maombi yetu?
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine

Sifa huja kutokana na moyo wa shukrani au furaha, pia unaweza ukaimba katika hali ya huzuni ukitoa hisia zako za ndani kutokana na kile unachopitia. Kuimba na kusifu ni vya muhimu kwa mafanikio ya ufahamu na mahusiano yako na Mungu, kabla haujaomba lazima ujiulize maswali kuwa je mahusiano yako yakoje na yule unayetaka kumuomba. Utimilifu wa kweli wa kiroho huja pale tunapoelekeza maisha yetu katika muendelezo wa kusifu na kuabudu, unapoendelea kumsifu na kumwabudu Mungu ndipo unaongeza ladha ya mahusiano yako ya kiroho na Mungu wako. Chanzo cha sifa zetu: Yesu ndio chanzo cha sifa zetu kwa sababu ya kile alichotutendea, alikufa msalabani kwa ajili yetu ili alipe deni zetu, alifufuka kutoka kaburini ili nasi tupate kuwa hai na sasa tuna fursa na uwezo wa kupokea miujiza mikuu ya Mungu kwa sababu ya kile alichofanya. Tunasifu na kuabudu kuheshimu na kushukuru kile Yesu alichokifanya kwa ajili yetu. Kuzaliwa upya kwa roho ya Mwanadamu kulikuja kupitia kile Ye...
Kuongozwa na Roho.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine

Kuongozwa na Roho. Maombi ni lazima, tumehimizwa na muumbaji kuomba, Kwa kila mwamini anapaswa kuwa na mambo yafuatayo:- 1. Afanye kazi, 2. Awe na umiliki juu ya nchi, 3. Azalishe, 4. Aombe, 5. Ashuhudie, 6. Aabudu, 7. Lazima awe mtoaji, 8. Lazima uwe na upendo, penda uumbaji, 9. Lazima asamehe na atubu, 10. Ahakikishe anatunza wito wake. Ukiyaweka haya pamoja ndipo unakuwa yule ambaye Mungu anampenda, 1 Wakorintho 2:10 “ Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. ” Mungu ametupa ufunuo kupitia roho wake, ufunuo ni nini? Maana yake ni kugundua mambo yaliyo sirini, maswala ya kiroho ukiyagundua yale yanayo ...