USHUHUDA ULIO HAI NI NGUVU YA MWAMINI
USHUHUDA ULIO HAI NI NGUVU YA MWAMINI Ushuhuda ni silaha ya nguvu dhidi ya adui zako. Ufunuo 12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.”Mungu alisema yeyote anayetaka uzima lazima atoe uhai wake lakini ukiuzuia uhai wako basi hauna uzima kwa maana ibilisi atakuharibu na kukuangamiza. Kutoa kuna nguvu sana, unapotoa uhai wako hapo ndipo nguvu ya mwamini ilipo. 1 Yohana 4:4 “Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.” Tunatokana na Mungu kwa jinsi gani? Kwa kupitia kuishi kwako, unapojitoa kwa Mungu inamaana kuwa unakuwa si wewe tena bali unakuwa ni mali ya Mungu. Pale unapokuwa ushuhuda ulio hai ndipo unakuwa na maisha ya utoshelevu, unakuwa mkuu kuliko wa ulimwengu, na kwa sababu hiyo unakuwa na haya:- • Hakuna anayeweza kukuangamiza kwa sababu wewe ulishakufa, • Magonjwa na maradhi hayawezi kukuangamiza kwa sababu uli...